Lugha Nyingine
Xi na Putin wasaini taarifa ya pamoja ya Mpango wa Maendeleo kabla ya Mwaka 2030
Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin Jumanne katika Ikulu ya Kremlin wamesaini na kutoa taarifa ya pamoja ya marais juu ya Mpango wa Maendeleo kabla ya Mwaka 2030 kuhusu Vipaumbele vya Ushirikiano wa Kiuchumi baina ya China na Russia.
Kwenye taarifa yao, pande hizo mbili zimekubaliana kushikilia kwa uthabiti kanuni za kuheshimiana, usawa na kunufaishana, kutimiza maendeleo ya kujitegemea ya muda mrefu ya nchi hizo mbili, kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya uchumi wa China na Russia na ushirikiano wa kibiashara, kuweka msukumo mpya kwenye kuhimiza kwa kina ushirikiano wa pande mbili, kuimarisha kasi ya ukuaji wa biashara ya pande mbili kwenye bidhaa na huduma, na kujitolea kuongeza kwa kiasi kikubwa biashara ya pande mbili hadi kufikia Mwaka 2030.
Mbali na hayo, pande hizo mbili pia zimedhamiria kuboresha ushirikiano wa kifedha, na kuongeza kwa utulivu matumizi ya sarafu za nchi hizo mbili kwenye biashara zao, uwekezaji, mikopo na miamala mingine ya kiuchumi na kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma