Lugha Nyingine
Rais Xi asema yuko tayari kuungana na Putin katika kupanga mipango ya uhusiano na ushirikiano wa kivitendo wa pande mbili
Rais wa China Xi Jinping amesema Jumanne kwamba yuko tayari kushirikiana na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, kupanga mipango ya uhusiano na ushirikiano wa kivitendo wa pande mbili ili kukuza maendeleo na ustawishaji wa nchi hizo mbili
Rais Xi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Putin katika hali ya kuongezwa kwa washiriki kwenye Ikulu ya Kremlin.
Rais Xi amesisitiza kuwa, kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Russia siku zote unadumisha kasi ya maendeleo yenye nguvu, afya na utulivu.
“Nchi hizo mbili zimezidisha kuaminiana kisiasa, maslahi ya pamoja na uhusiano kati ya watu na watu, na zimeendelea kuendeleza ushirikiano katika uchumi, biashara, uwekezaji, nishati, mabadilishano ya watu na utamaduni pamoja na ushirikiano katika ngazi ya serikali za mitaa” Rais Xi amesema.
Ameeleza kuwa tangu awasili Moscow amekuwa na mazungumzo mazuri na Rais Putin na Waziri Mkuu Mikhail Mishustin, na kufikia makubaliano mengi muhimu nao.
“Ushirikiano kati ya China na Russia unahusisha maeneo mengi zaidi, kujenga maelewano zaidi na kutoa manufaa ya mapema,” Rais Xi amesema, huku akibainisha kuwa ushirikiano zaidi unaendelezwa kikamilifu.
Alieleza kuwa China iko katika mwaka wa kwanza wa kutekeleza kikamilifu mipango na maagizo elekezi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na China itakuza dhana mpya ya maendeleo kwa kasi ya haraka, kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu, na kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China katika mambo yote.
Rais Xi ameeleza utayari wake wa kufanya kazi na Putin kutoa mwongozo na maagizo kwa uhusiano na ushirikiano wa kivitendo wa pande mbili ili kukuza maendeleo na ustawishaji wa nchi zote mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma