Lugha Nyingine
Mkurugenzi Mtendaji katika Benki ya HSBC asema China inatoa fursa za kuvutia kwa kampuni na wawekezaji wa kigeni
Picha hii iliyopigwa Tarehe 13 Machi 2023 ikionyesha kituo cha kontena cha Bandari ya Taicang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Bo)
LONDON - Uchumi wa China unatoa fursa za ukuaji wa muda mrefu na fursa za kuvutia kwa kampuni na wawekezaji wa kigeni, amesema Nuno Matos, Mkurugenzi Mtendaji wa Wealth and Personal Banking, chini ya Benki ya HSBC, katika mahojiano yaliyochapishwa hivi karibuni na Shirika la Habari la Xinhua.
Matos amesema kwamba tukiangalia nyuma kuanzia Mwaka 2022, masoko ya China na Asia yameonyesha uhimilivu mkubwa, na kufufuka kwa uchumi wa China kutokana na athari za janga la UVIKO-19 "kunatokea kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa, na kuweka msingi thabiti wa Mwaka 2023."
Amesema hivi karibuni Benki ya HSBC imepandisha makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa China hadi asilimia 5.6 Mwaka 2023 kutoka asilimia 5.0 ya awali huku ikitarajiwa kwamba kurejea kwa uimara kwa matumizi katika manunuzi kuwa kichocheo kikuu cha ukuaji wa uchumi nchini China, hususan katika sekta ya huduma.
Benki ya HSBC pia inatarajia utajiri wa familia nchini China kukua kwa karibu asilimia 8.5 kila mwaka katika miaka michache ijayo, na mali za familia zinazoweza kuwekezwa zitazidi thamani ya Yuan trilioni 300 (kama dola trilioni 43.5 za Kimarekani) ifikapo Mwaka 2025, "ikitoa msingi mzuri wa utajiri kwa maendeleo ya jamii za China. "Matos amesema.
Mtaalam huyo wa masuala ya benki anaamini kuwa uwekezaji wa kigeni unaweza kuwa na mchango muhimu katika kuendeleza masoko ya fedha yenye kuunga mkono uhifadhi wa mazingira na kwamba "kina cha masoko ya mitaji ya China kinasisitiza azma yake ya kuwa kiongozi wa kimataifa katika nafasi hii."
Picha hii iliyopigwa Januari 31, 2023 ikionyesha magari yatakayowasilishwa katika eneo la maegesho la Kampuni ya FAW Jiefang huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Xu Chang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma