Lugha Nyingine
Msemaji: Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia moja lahimiza ukuaji wa uchumi, kuboresha maisha ya watu
Guo Weimin, msemaji wa mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, akishiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, China Tarehe 3, Machi. (Picha/Xinhua)
Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limehimiza ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu katika nchi zinazoshiriki, alisema msemaji wa CCPPC Ijumaa wiki iliyopita.
Ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia moja umeleta uwekezaji wenye ufanisi na miundombinu mingi zaidi yenye ubora kwa nchi zinazoshiriki, alisema Guo Weimin, msemaji wa mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mwaka huu utatimiza mwaka wa 10 wa maadhamisho ya Ukanda Mmoja, Njia Moja. Hadi katikati mwa Februari mwaka huu, China imetia saini makubaliano ya kushirikiana pamoja na nchi 151 na mashirika 32 ya kimataifa, na thamani ya biashara yake na nchi pembezoni mwa Ukanda Mmoja, Njia Moja imeongezeka mara dufu kutoka 2013 hadi 2022, alisema Guo.
Akijibu kile kinachoitwa “mitego ya deni”, Guo amesema “kelele” hizi hazina msingi.
China imetilia sana maanani kukwepa kusababisha hatari ya deni kwenye utekelezaji wa BRI, na imehimiza mfumo wa uwekezaji na ufadhili ambao ni thabiti, endelevu na wa muda mrefu ili kuhakikisha hatari inakuwa chini ya udhibiti, alisema Guo.
Guo alisema, China itatumia fursa ya maadhimisho ya mwaka wa 10 wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kutoa zaidi nishati mpya na nafasi ya ushirikiano wa kimataifa wa uchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma