Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa rais aliyechaguliwa wa Nigeria Tinubu
Tarehe 4, Machi, Rais Xi Jinping wa China alimtumia simu Bola Tinubu kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa rais wa Jumhuri ya Shirikisho la Nigeria.
Rais Xi Jinping alisema, Nigeria ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa China kwenye Bara la Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni iliyopita, mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mzuri, na ushirikiano wao wa kivitendo katika sekta mbalimbali umepata matunda kemkem. Nchi hizo mbili zimeungana mkono katika masuala yanayohusiana na maslahi yao ya kimsingi na masuala makubwa yanayofuatiliwa nao, na kushirikiana kwa karibu kwenye mambo ya kimataifa na ya kikanda. Ninatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Nigeria, na ningepenga kufanya juhudi pamoja na rais Tinubu, ili kusukuma uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili uendelee kwenye ngazi ya juu zaidi siku hadi siku.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma