Lugha Nyingine
Benki Kuu ya Iraq yatangaza kuruhusu biashara zifanywe mahesabu kwa fedha za Renminbi moja kwa moja
(Picha inatoka ChinaDaily.)
Benki Kuu ya Iraq tarehe 22 ilitangaza hatua mpya za kuboresha akiba ya fedha za kigeni, ikiwemo hatua ya kuruhusu biashara kati ya nchi hiyo na upande wa China zifanywe mahesabu kwa fedha za Renminbi moja kwa moja.
Mshauri wa masuala ya uchumi wa serikali ya Iraq Mudhir Salih aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Iraq kuruhusu biashara za uingizaji bidhaa kutoka China zifanywe mahesabu kwa kutumia fedha za Renminbi moja kwa moja, na hapo kabla biashara za aina hiyo na China siku zote zilifanywa mahesabu kwa Dola za Marekani.
China ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara kwa Iraq, na Iraq ni mwenzi mkubwa wa tatu wa biashara kwa China miongoni mwa nchi za Kiarabu.
Tovuti ya habari ya Mashariki ya Kati “Al-Monitor” ilisema, hatua ya benki kuu ya Iraq imeonesha zaidi kuwa, baadhi ya nchi za mashariki ya kati “zinazikimbia Dola za Marekani”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma