Lugha Nyingine
Makampuni ya China yatafuta ushirikiano zaidi wa kikanda kupitia maonyesho makubwa zaidi ya mafuta nchini Misri
Picha iliyopigwa Februari 13, 2023 ikionyesha banda la Kampuni ya Mafuta ya China ZhenHua kwenye Maonyesho ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) mjini Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Picha iliyopigwa Februari 13, 2023 ikionyesha Banda la Kampuni ya Teknolojia ya Huawei ya China kwenye Maonyesho ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) mjini Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Watu wakitembelea banda la Kampuni ya Teknolojia ya Huawei ya China kwenye Maonyesho ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) huko Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Mtembeleaji akizungumza na muonyeshaji kwenye Banda la Kampuni ya Mafuta ya China ZhenHua kwenye Maonyesho ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) mjini Cairo, Misri, Februari 13, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Watu wakitembelea Banda la Kampuni ya Mafuta ya Zhenhua ya China kwenye Maonyesho ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) mjini Cairo, Misri, Februari 13, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
CAIRO - Makampuni ya mafuta na teknolojia ya China yamewavutia watembeleaji wengi kwenye Maonyesho Sita ya Mafuta ya Petroli ya Misri (EGYPS) yanayoendelea, ambayo ni maonyesho makubwa zaidi ya mafuta katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ambayo yamekusanya waonyeshaji bidhaa na huduma wa makampuni zaidi ya 500 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
"Tunaichukulia Misri kama kituo kikuu cha kutafuta fursa zetu za biashara hapa katika eneo la Mashari ya Kati na Afrika Kaskazini na Bara la Afrika," anasema Ma Cheng, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Petroli ya Kaskazini (NPIC) S.A., ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mafuta ya Zhenhua ya China.
Ikiwa na banda linalovutia watembeleaji wengi katika maonyesho hayo, Kampuni ya Mafuta ya Zhenhua inajivunia uzoefu wake wa miaka tisa katika uendeshaji wa maeneo ya mafuta na gesi nchini Misri na kutengeneza fursa za ajira 1,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Wamisri.
"Kupitia maonyesho haya, tuko tayari kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu wa Misri," ameeleza, huku akiongeza kuwa biashara za kampuni hiyo nchini Misri ni sehemu ya matunda ya Mpango wa Ukanda Mmoja, Njia Moja unaopendekezwa na China ambao unalenga kukuza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi zinazoshiriki.
NPIC na Shirika la Kimataifa la Petroli la Misri zilianzisha ubia wa Kampuni ya Petro Amir Petroleum ili kuzalisha mafuta na gesi katika maeneo matatu katika Jangwa la Mashariki na Magharibi nchini Misri.
"Ninaamini kuwa China ni mshirika mkuu wa uwekezaji wa Misri ... ikiwa ni pamoja na katika sekta ya mafuta," amesema mwanajiolojia wa Misri Samir Zalat, ambaye ni Meneja Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Petro Amir Petroleum.
Zaidi ya makampuni 500 kutoka nchi mbalimbali duniani yameshiriki katika maonyesho hayo, yakiwemo makampuni ya Misri, Italia, Marekani, Uingereza, India, Cyprus, Ugiriki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uturuki, Hispania na China.
Miongoni mwa makampuni waonyeshaji kutoka China ni kampuni mashuhuri ya Huawei, yenye banda lake linalotambulisha suluhu mbalimbali za teknolojia za habari na mawasiliano (TEHAMA).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma