Lugha Nyingine
Benki ya Dunia yasema uchumi wa Tanzania wazidi kuimarika
Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania inaonesha kuwa Pato la Taifa (GDP) la Tanzania linatarajia kupanda kutoka asilimia 4.6 za mwaka jana hadi asilimia 5.3 mwaka huu.
Sehemu ya ripoti hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imetaja sababu zilizochangia kukua kwa uchumi wa Tanzania kuwa ni pamoja na kufunguliwa kwa shughuli za utalii na mipaka kwa shughuli za kiuchumi na mafanikio katika utoaji chanjo dhidi ya COVID-19, hali iliyofungua sekta za biashara na uzalishaji.
Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imesifu misingi ya kiuchumi ya Tanzania kuhimili misukosuko ya kiuchumi iliyoziathiri nchi nyingi za Afrika kutokana na janga la COVID-19 ambalo lilizorotesha uchumi wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Hata hivyo ripoti hiyo imesema mlipuko wa COVID- 19 umesababisha kiwango cha umaskini kuongezeka kutoka asilimia 21 Mwaka 2019 hadi asilimia 26 Mwaka 2021 kwa nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja na Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma