Lugha Nyingine
Mwekezaji wa China aelezea imani yake kwenye soko la Ghana
ACCRA - Mwekezaji mkuu wa China nchini Ghana Jumapili alionyesha imani yake kubwa kwenye soko la Ghana licha ya matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Tang Hong, Mwenyekiti wa Shirikisho la Jumuiya za Wachina nchini Ghana, ametoa maoni yake katika hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la majina ya wafanyabiashara wa China nchini Ghana.
Tang ameeleza kuwa kuzorota kwa mazingira ya biashara kunakotokana na mfumuko wa bei na kuendelea kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi hiyo kumesababisha matatizo kwa baadhi ya biashara za China.
“Pamoja na matatizo na changamoto kubwa, kiwango cha biashara kati ya China na Ghana kilishuhudia ukuaji katika miezi 11 ya kwanza mwaka jana, na idadi ya wataalamu wahamiaji kutoka China waliosajiliwa nchini Ghana ni kubwa kuliko wale waliosajiliwa katika nchi nyingine yoyote,” amesema.
"Ishara zote zinaonyesha wawekezaji wa China wana imani kubwa kwa soko la Ghana," Tang amesema.
Ameeleza kuwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China, pamoja na Mpango wa Kiwanda kimoja, Wilaya Moja wa Ghana, vimechangia kwa kiasi kikubwa maendekeo ya viwanda nchini Ghana na kuinua viwango vya maisha vya Waghana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma