Lugha Nyingine
Kuanzia Februari China itarejesha kwa majaribio biashara ya Mashirika ya Utalii ya utalii wa nje
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2023
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)
Ofisi ya Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China imetoa “Uarifu kuhusu Kurejesha kwa Majaribio biashara ya Mashirika ya Utalii ya utalii katika nchi husika kwa makundi ya raia ”. Uarifu huo unafafanua kuwa, kuanzia Tarehe 6, Februari, 2023, mashirika ya utalii na mashirika ya mtandaoni ya utalii kote nchini China yatarejesha kwa majaribio biashara ya utalii wa nje wa watu wa China kwa vikundi na kuagiza “Tiketi ya Ndege + Hoteli” katika nchi husika. Nchi hizo ni : Thailand, Indonesia, Cambodia, Maldives, Sri Lanka, Filipino, Malaysia, Singapore, Laos, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Kenya, Afrika Kusini, Russia, Uswiss, Hungary, New Zealand, Fiji, Cuba, na Argentina.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma