Lugha Nyingine
Filamu mpya zilizooneshwa wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China zaonyesha imani ya kitamaduni ya watu wa China
Picha hii iliyopigwa Januari 23, 2023 ikionyesha watu wakiwa kwenye ukumbi wa sinema huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Li Yibo)
BEIJING - Watu wa China waliosherehekea sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China mwaka huu wamekaribishwa vizuri na filamu kadhaa mpya zinazoonyesha imani ya kitamaduni, zikiwa na ari ya umaalum wa China na kuwavutia watazamaji wengi.
Filamu hizo, zikiwemo "Full River Red" na "The Wandering Earth II," zinaonyesha kwa Dunia uzalendo, umoja, ushujaa na umaalumu wa kitaifa walionao watu wa China na Taifa la China. Wakati wa likizo hiyo iliyomalizika hivi punde, filamu hizo, hazikuboresha tu maisha ya kiroho ya watu, lakini pia zimeunganisha watu moyoni na akilini.
Wakati wa likizo ya wiki nzima ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo ilimalizika Ijumaa iliyopita, mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi kwa ajili ya kutazama filamu nchini China yalifikia karibu yuan bilioni 6.76 (kama dola bilioni 1 za Kimarekani), ikiwa ni takwimu zinazoweka rekodi ya kuwa nafasi ya pili kwa juu zaidi katika historia ya utazamaji filamu wakati wa likizo hiyo. Filamu mbili zilizo katika nafasi ya juu kwa kutazamwa zaidi ni "Full River Red" na ile ya sci-fi "The Wandering Earth II," ambazo zimeingiza takriban yuan bilioni 2.61 na zaidi ya yuan bilioni 2.16, mtawalia.
Filamu ya Vichekesho ya "Full River Red" iliyoongozwa na mwongozaji maarufu wa filamu Zhang Yimou inasimulia hadithi ya kuondoa uovu ili kuonyesha uaminifu na kufuata haki. Filamu hiyo ilieleza hadithi ya mhusika Yue Fei, ambaye alikuwa kamanda wa kijeshi mzalendo wa Enzi ya Song ya Kusini (1127-1279), ambaye alipigana vita dhidi ya Enzi ya Jin (1115-1234).
Ye Hang, profesa mshiriki wa Chuo cha Filamu cha Beijing, ameeleza kuwa wahusika katika filamu hiyo wanafuatilia ukweli wa mambo, na kushikilia maadili na uadilifu. Amesema, hisia za uzalendo na kasi kuu iliyomo katika filamu hiyo ni ya kimhemko na ya kutia moyo, huku ikifichua thamani na maana ya maisha, hisia ambazo zimesifiwa na watu vizazi hadi vizazi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma