Lugha Nyingine
Uchumi wa China wajitokeza wasimama imara duniani
Picha hii iliyopigwa Januari 17, 2023 ikionesha mandhari ya asubuhi kwenye Eneo la Bandari ya Jingtang kwenye Bandari ya Tangshan, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China.(Picha na Liu Mancang/Xinhua) |
BEIJING - Katika mapambano yake ya miaka mitatu dhidi ya UVIKO-19, China ilirekodi matokeo bora katika maendeleo ya kiuchumi na udhibiti wa janga, na kuimarisha nafasi yake duniani ya kuwa injini inayoongoza kwa uchumi wa Dunia.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi wa Kitaifa wa Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Yuan Da amesema, kuanzia Mwaka 2020 hadi 2022, wastani wa ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka ni asilimia 4.5 kuliko wastani wa Dunia wa karibu asilimia 2.
Mwaka 2022, ongezeko la uchumi wa China lilifikia asilimia 3 kuliko lile la mwaka 2021 na kuweka rekodi ya juu ya yuan trilioni 121 (karibu dola trilioni 18 za Kimarekani), huku ongezeko likiwa yuan trilioni 6.1, sawa na jumla ya utoaji uchumi wa nchi yenye mapato ya kati.
Wachambuzi wa mambo ya uchumi, wanahusisha matokeo yaliyopatikana kwa bidii na uratibu madhubuti wa China katika kupambana na UVIKO-19 na athari zake kiuchumi kwa wakati mmoja.
Kuzuia Virusi vya Korona
Ili kukabiliana na hali ya janga inayoendelea kubadilika, China imekuwa ikiboresha hatua zake za udhibiti huku ikiimarisha uwezo wa huduma za afya na utoaji chanjo, kulinda maisha na afya ya wakazi wake bilioni 1.4 kwa gharama ndogo.
Hadi kufikia Januari 13, asilimia 92.9 ya watu wa China wamepatiwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya Korona, huku zaidi ya asilimia 90 ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wakipata chanjo.
Ustawi wa kiuchumi
Katika likizo iliyohitimishwa hivi punde ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, matumizi ya China kwenye ununuzi yamerejesha nguvu ya uchumi.
Wakati wa likizo hiyo ya wiki nzima, mapato yatokanayo na mauzo kwenye sekta zinazohusiana na matumizi ya China yalipanda kwa asilimia 12.2 kutoka kipindi kama hicho cha likizo Mwaka 2022.
Wen Bin, mchumi mkuu wa Benki ya Minsheng ya China, amesema kuwa kuongezeka kwa mahitaji kunachochea mabadiliko katika uchumi wa China mwaka huu na kukadiria ukuaji wa Pato la Taifa la mwaka mzima wa karibu asilimia 5.5.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma