Lugha Nyingine
Mji wa Shanghai nchini China waanzisha mpango kazi wa kuleta utulivu kwenye ukuaji wa uchumi na kuhimiza maendeleo
Picha hii iliyopigwa Tarehe 4 Novemba 2022 ikionyesha mandhari ya jioni kwenye eneo la Lujiazui huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Xiang)
SHANGHAI - Serikali ya Mji wa Shanghai, China Jumapili ilitangaza kuanzisha mpango kazi wa kupanua mahitaji, kuleta utulivu kwenye ukuaji wa uchumi na kuhimiza maendeleo.
Chini ya mpango huo, unaojumuisha sera na hatua 32, mji huo mkubwa ulioko Mashariki mwa China utatekeleza kikamilifu sera zenye nafuu kwa kodi, ikiwa ni pamoja na msamaha wa kodi kwenye ununuzi wa magari yanayotumia nishati mpya.
Wakati huo huo, hatua zitachukuliwa ili kupunguza gharama za ajira kwa makampuni ya biashara.
Ili kurejesha na kuongeza matumizi katika ununuzi, Shanghai itatoa ruzuku kwa watumiaji wanaonunua vyombo vya umeme nyumbani vya akili bandia bila kutoa uchafuzi kwa mazingira. Pia itatoa kuponi za utalii wa kitamaduni, michezo, huduma za vyakula na matumizi ya rejareja.
Tokea Mwaka 2023, Shanghai imesaini makubaliano kuhusu zaidi ya miradi 160 muhimu ya viwanda, na uwekezaji yenye thamani ya jumla inayofikia yuan bilioni 100 (takriban dola bilioni 14.77 za Kimarekani).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma