Lugha Nyingine
Takwimu za ushuru zaonyesha ukuaji wa matumizi katika wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Watu wakinunua vitu kwenye duka lisilotozwa ushuru la Haikou Riyue Plaza huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Januari 25, 2023. Watalii walienda kufanya manunuzi katika Mkoa wa Hainan, ambao ni kivutio kikuu cha watalii wakati wa majira ya baridi kali, wakati wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China. (Xinhua/Yang Guanyu)
BEIJING - Mapato yanayotokana na mauzo kwenye sekta zinazohusiana na matumizi ya China wakati wa likizo ya wiki moja ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yaliongezeka kwa asilimia 12.2 kuliko yale ya mwaka jana, takwimu za kodi zimeonyesha Ijumaa.
Kwa mujibu wa takwimu za kodi ya nyongeza za thamani zilizotolewa na Idara ya Kodi ya kitaifa ya China, mapato yanayotokana na mauzo yameshuhudia wastani wa ongezeko wa mwaka wa asilimia 12.4 ukilinganishwa na kipindi kama hicho wakati wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ya Mwaka 2019, kipindi cha kabla ya UVIKO-19.
Ufufukaji wa huduma za utalii na malazi umeharakishwa. Mapato yatokanayo na mauzo ya mashirika ya utalii na huduma zinazohusiana yaliongezeka kwa asilimia 130 wakati wa likizo kuliko ule wa likizo iliyopita ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na kufikia asilimia 80.7 wakati wa likizo kama hiyo ya Mwaka 2019, takwimu zimeonyesha.
Hoteli za kitalii na minyororo ya hoteli imeshuhudia mapato yatokanayo na mauzo yakiongezeka kwa asilimia 16.4 na asilimia 30.6 kuliko mwaka jana.
Wakati huo huo, matumizi ya mahitaji ya kila siku yamedumisha ukuaji thabiti, huku mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za msingi kama vile nafaka, mafuta na chakula yakiongezeka kwa asilimia 31.5 kuliko yale ya likizo iliyopita ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyoanza Januari 21 mwaka huu, ambapo ni wakati muhimu zaidi wa kujumuika kwa watu wa familia mojamoja nchini China na linaashiria mwanzo wa majira ya mchipuko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma