Lugha Nyingine
Zaidi ya safari milioni 300 zashuhudiwa nchini China wakati wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Abiria wakipita ukaguzi wa tiketi katika Stesheni ya Reli ya Nanning Mashariki huko Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Januari 27, 2023. Stesheni za reli, barabara kuu na viwanja vya ndege kote China vinashuhudia pilikapilika mpya za usafiri wa watu wanaorudi kazini baada ya likizo ya wiki nzima ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ambayo imekamilika jana Ijumaa. (Xinhua/Lu Boan)
BEIJING - Takriban safari milioni 308 zimefanywa kote nchini China wakati wa likizo ya mwaka huu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.1 kuliko mwaka jana , imesema Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China.
Mapato ya utalii wa ndani yaliyopatikana wakati wa likizo hiyo ya wiki nzima yamefikia yuan bilioni 375.8 (karibu dola za Kimarekani bilioni 55.52), ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kuliko yale ya mwaka jana , takwimu kutoka wizara hiyo zimeonyesha.
Jumla ya vivutio vya utalii 10,739 vya kiwango cha Daraja A, ambavyo vinawakilisha asilimia 73.5 ya vile vya jumla vya kote nchini China, vilifunguliwa kama kawaida wakati wa likizo.
Wakati wa likizo hiyo, shughuli mbalimbali za kitamaduni na kitalii pia zilifanyika nchi nzima ili kuchochea matumizi ya usiku, imesema wizara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma