Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Bob Dadae kwa kuchaguliwa tena kuwa Gavana Mkuu wa Papua New Guinea
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa iliyopita alimpongeza Bob Dadae kwa kuchaguliwa tena kuwa Gavana Mkuu wa Papua New Guinea (PNG).
Katika ujumbe wake, Rais Xi amesema, Papua New Guinea ni moja ya nchi za visiwa vya Pasifiki zilizoanzisha mapema zaidi uhusiano wa kidiplomasia kati yao na Jamhuri ya Watu wa China, na nchi hizo mbili zinafurahia kudumisha urafiki.
Rais Xi amesema, hivi sasa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Papua New Guinea umekuwa ukiendelezwa kwa kiwango cha juu katika mawasiliano na ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali, na kuleta manufaa makubwa kwa watu wa pande hizo mbili.
Huku akieleza kwamba anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Papua New Guinea, na yuko tayari kuendelea kushirikiana na Dadae ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana siku za nyuma na kusonga mbele kwa ukuaji thabiti na endelevu wa uhusiano wa pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma