Lugha Nyingine
Uchumi wa China watarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa kikanda Mwaka 2023
(CRI Online) Januari 28, 2023
(Picha inatoka CRI.)
Uchumi wa China unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.8 kwa mwaka huu kufuatia serikali nchini kuboresha hatua za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, kuchukua hatua za kuchochea ukuaji wa uchumi pamoja na ongezeko la mahitaji ya ununuzi kwa watu wa China.
Hayo yamo kwenye ripoti ya hali ya uchumi wa dunia na makadirio kwa Mwaka 2023 iliyotolewa Tarehe 25 na Umoja wa Mataifa ambayo pia imekadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa China utakuwa asilimia 4.8 kwa Mwaka 2023, na kwamba ufufukaji wa uchumi wa China utachangia ukuaji wa kanda nzima.
Ripoti hiyo pia imesema Mwaka 2023 ukuaji wa uchumi wa Umoja wa Ulaya, Marekani na Japan utakuwa asilimia 0.2, 0.4 na 1.5 mtawalia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma