Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Nepal kutokana na ajali ya ndege
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2023
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatatu alituma ujumbe wa rambirambi kwa Rais wa Nepal Bidya Devi Bhandari kutokana na ajali ya ndege nchini humo.
Katika ujumbe wake, Rais Xi amesema baada ya kupata habari kuhusu ajali ya ndege iliyotokea nchini Nepal na kusababisha hasara kubwa, akiwa kwa niaba ya serikali na watu wa China anatoa rambirambi za dhati zaidi kwa vifo vya watu kwenye ajali na kutoa pole za dhati kwa familia zilizofiwa.
Pia siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang alituma ujumbe wa rambirambi kwa Waziri Mkuu wa Nepal Pushpa Kamal Dahal.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma