Lugha Nyingine
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuanzisha benki kuu ya kikanda mwaka huu
(CRI Online) Januari 17, 2023
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dk. Peter Mathuki amesema uamuzi wa kuanzisha Benki Kuu ya Afrika Mashariki utafanywa mwaka huu, hatua ambayo ni muhimu katika kutekeleza utaratibu wakutumia sarafu ya pamoja.
Dk. Mathuki amesema Baraza la Mawaziri linatarajiwa kupanga kuhusu eneo la kujengwa kwa Benki hiyo mwaka huu. Hivi karibuni nchi wanachama zimekuwa zikijitahidi kuwa mwenyeji wa benki hiyo, kila moja ikitafuta kujipatia uwezo mkubwa wa kuvutia mitaji ya kigeni na kuwa kitovu cha kifedha cha jumuiya.
Sarafu ya pamoja ya nchi hizi itarahisisha biashara na usafiri wa watu ndani ya eneo hilo, jambo ambalo litafanikisha lengo la Jumuiya hiyo kama linavyoelezwa katika Itifaki ya Soko la Pamoja.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma