Lugha Nyingine
Mji wa Beijing nchini China wachochea matumizi kufuatia hatua bora za kudhibiti UVIKO
Mtu akinunua tiketi za kutazama filamu kwenye jumba la sinema lililopo kwenye kituo cha maduka makubwa hapa Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 25, 2022. (Xinhua/Ren Chao)
BEIJING – Mji wa Beijing nchini China umeweka lengo la ukuaji wa Pato la Jumla la Mji (GDP) kwa zaidi ya asilimia 4.5 kwa Mwaka 2023, na kuahidi kuchochea zaidi matumizi katika ununuzi wa bidhaa katika wakati wa kufufua ukuaji wa uchumi, amesema Kaimu Meya wa mji huo Yin Yong.
"Kurejesha na kupanua matumizi kunapaswa kuwa kipaumbele," Yin amesema Jumapili alipokuwa akitoa ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Mji wa Beijing.
Mji mkuu huo wa China uliahidi kujenga mazoea ya matumizi katika tasnia ya kidijitali, utamaduni, na michezo kwenye barafu na theluji na kusaidia matumizi katika uboreshaji wa makazi, magari yanayotumia nishati mpya, na huduma za kuwatunza wazee ili kufufua uchumi, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kazi ya serikali iliyotolewa.
Ili kutumia vizuri fursa ya mchango wa uwekezaji katika kuboresha muundo wa utoaji , Beijing itatilia maanani zaidi miradi 100 ya miundombinu, miradi 100 ya kuboresha maisha ya watu, na miradi 100 ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na tasnia ya teknolojia ya hali ya juu, imesema ripoti hiyo.
“Beijing itaongeza kufungua mlango na mageuzi katika kiwango cha juu ili kuongeza imani ya soko,” Yin amesema, na kuongeza kuwa mji huo utaharakisha urejeshaji wa usafiri wa ndege za abiria wa kimataifa na kuongeza njia za usafiri wa ndege za mizigo wa kimataifa.
Mji huo pia umeweka malengo ya viashiria vingine vikuu vya kiuchumi Mwaka 2023, ikiwa ni pamoja na kiwango cha asilimia 5 au chini cha ukosefu wa ajira mjini kilichofanyiwa uchunguzi na ukuaji wa fahirisi ya bei ya wanunuzi (CPI) kwa takriban asilimia 3, imesema ripoti hiyo ya kazi ya serikali.
Kwa kuendelea kuboreshwa kwa sera za kuzuia na kudhibiti UVIKO-19, uchumi wa Mji wa Beijing umefufuka hatua kwa hatua kutokana na athari mbaya ya janga hilo, na kurejesha msongamano wake wa kawaida, na kuwa mfano miongoni mwa miji ya China.
Hong Tao, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Teknolojia na Biashara cha Beijing, amesema soko la watumiaji nchini China linatarajiwa kufufuka mwaka huu, na kutoa mahitaji yaliyomo ambayo hapo awali yalizuiwa na janga la UVIKO-19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma