Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping na mwenzake wa Angola wapongezana kwa kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China Alhamisi na Rais wa Angola Joao Lourenco walitumiana salama za pongezi kwa kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi katika salama zake amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 40 iliyopita, China na Angola siku zote zimekuwa udhati na urafiki kati yao, zimefanya kazi bega kwa bega, na kuelewana na kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi na mambo muhimu yanayofuatiliwa kwa pamoja.
Rais Xi amesema hivi sasa uhusiano kati ya China na Angola unafuata mwelekeo mzuri wa maendeleo, na ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali umekuwa na matokeo mazuri, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa watu wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema anathamini sana maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili, na yuko tayari kushirikiana na Lourenco kutumia maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia kama fursa ya kuimarisha kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande mbili na kuandika ukurasa mpya katika maendeleo thabiti ya ushirikiano wa kimkakati wa China na Angola.
Kwa upande wake, Rais Lourenco amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, uhusiano kati ya Angola na China umekuwa na maendeleo siku hadi siku, na ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa yenye matokeo ya kuridhisha.
Akibainisha kuwa nchi hizo mbili zinakubaliana katika masuala mengi ya kimataifa, Rais Lourenco amesema Angola iko tayari kuimarisha uhusiano na urafiki na ushirikiano na China, kujenga manufaa ya pamoja yenye mustakabali wa baadaye, vilevile kupata mafanikio, ustawi na maendeleo ya pamoja, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma