Lugha Nyingine
Mkurugenzi wa Baraza la Utalii Duniani asema sekta ya utalii duniani kupata nguvu kutokana na wasafiri wa China
Abiria wa China wakikaribishwa na maafisa wa Thailand katika Uwanja wa Ndege wa Suvarnabhumi wa Samut Prakan, Thailand, Januari 9, 2022. (Xinhua/Rachen Sageamsak)
GENEVA - Ofisa Mtendaji Mkuu (Mkurugenzi Mtendaji) wa Baraza la Usafiri na Utalii Duniani (WTTC) ameelezea matumaini yake juu ya kufufuka kwa sekta hiyo kutokana na janga la UVIKO-19 na anatarajia ukuaji wa kasi katika muongo ujao hasa kutokana na kuongezeka kwa wasafiri wa China na wageni watakaotembelea China.
Abiria wakiwa kwenye foleni ya ukaguzi wa kiusalama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Haikou Meilan wa Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Januari 7, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
"Nimekuwa huko (China) mara nyingi ... na ni habari njema ya kushangaza kwamba Dunia itaweza kufungua mikono yake na kuwakaribisha tena watalii wa China," Julia Simpson, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa WTTC, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni ya video.
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Usafiri na Utalii Duniani (WTTC) Julia Simpson akizungumza jukwaani kwenye Mkutano wa Kimataifa wa WTTC katika Jiji la Pasay, Ufilipino Tarehe 21 Aprili 2022. (Xinhua/Rouelle Umali)
"Safari za kulipiza"
Likiwa ni shirika lisilo la faida, wanachama wa WTTC wanajumuisha zaidi ya Wakurugenzi Wakuu 200, wenyeviti na marais wa sekta binafsi zinazoongoza duniani za biashara za usafiri na utalii.
Simpson amesema kuwa karibu miaka mitatu imepita, hali ya "safari za kulipiza kisasi", ambayo inamaanisha kusafiri kwa lengo la kulipia wakati uliopotea kipindi cha janga hilo, inatarajiwa kuinua utalii na kukuza biashara.
Wasafiri wa China waliotembelea sehemu nyingine za Dunia walikuwa "miongoni mwa watu wa thamani zaidi kwa maana ya kiuchumi," Simpson amesema.
Kwa mujibu wa WTTC, Mwaka 2019, wageni hao wa China walitumia dola bilioni 253 za kimarekani duniani kote, thamani ambayo iliwakilisha asilimia 15 ya jumla yote.
Watalii wa China wakipiga picha mbele ya Arc de Triomphe mjini Paris, Ufaransa, Machi 20, 2019. (Xinhua/Gao Jing)
Maeneo muhimu ya kutembelea
Simpson amesema, kwa wasafiri kutoka China, nchi za Maldives na Mauritius, Australia na New Zealand, Ulaya na Marekani ndizo zinaongoza kwenye orodha ya juu ya Wachina wengi kutembelea.
"Ninaweza kueleza hapa ni duniani kote, kwa sababu, kwa kweli, watalii wa China sasa wako kila mahali," amesema.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema, vivutio kama vile Ukuta Mkuu, miji ya Chengdu au Guilin vinaweza kuwavutia wasafiri wa nchi mbalimbali kwenda China.
Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2023 ikionyesha mandhari ya machweo ya jua kwenye sehemu ya Simatai ya Ukuta Mkuu wa China katika Eneo la Miyun la Beijing, China. (Xinhua/Xing Guangli)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma