Lugha Nyingine
Uchumi wa Kenya unakadiriwa kukua kwa asilimia 6.1 mwaka 2023
(CRI Online) Januari 05, 2023
Wizara ya Fedha ya Kenya imetoa ripoti ya makadirio ya ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, ikisema uchumi wa Kenya utafufuka kwa asilimia 6.1 mwaka 2023.
Katika ripoti yake iliyotolewa baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya Agosti, 2022, Hazina hiyo ilisema ongezeko la uchumi wa nchi hiyo litafikia asilimia 5.5.
Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Njuguna Ndung’u amesema miradi mipya ya uchumi ya serikali inalenga kuongeza uwekezaji katika sekta tano zinazoonekana kuwa na athari kubwa katika uchumi na pia ustawi wa familia. Amezitaja sekta hizo kuwa ni kilimo, viwanda vidogo, na vya ukubwa wa kati, nyumba na makazi, afya na maendeleo ya dijitali, na sekta ya uvumbuzi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma