Lugha Nyingine
Marais wa China na Ufilipino wafanya mazungumzo
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)
Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr ambaye yuko ziarani nchini China katika Jumba la Mikuano ya Umma mjini Beijing.
Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Ufilipino, kuendelea kushughulikia masuala ya baharini kupitia njia ya mazungumzo, kurejesha mazungumzo ya uendelezaji wa mafuta na gesi, na kuanzisha ushirikiano wa nishati kijani.
Kwa upande wa rais Marcos Jr, amesisitiza kuwa Ufilipino inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kwamba nchi yake itaendelea kushughulikia kirafiki na kwa kufaa matatizo kwenye baharini na China.
Baada ya mazungumzo hayo, marais hao wawili walishuhudia pamoja kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, sekta ya kilimo na uvuvi, miundombinu, mambo ya fedha, forodha, biashara ya kielektroniki na utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma