Lugha Nyingine
China yashuhudia kufufuka kwa matumizi katika Mwaka Mpya, yajipanga kukuza uchumi Mwaka 2023
BEIJING – Huku China ikiwa imekamilisha na kulegeza hatua za kukabiliana na UVIKO-19, nchi hiyo pia imepanua usambazaji wa bidhaa na mahitaji ili kuongeza matumizi kwenye manunuzi katika mwaka mpya.
Likizo ya siku tatu ya Mwaka Mpya imeshuhudia kufufuka kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za utalii, huduma za chakula na mauzo ya rejareja kote nchini China.
Katika siku ya mwisho ya Mwaka 2022, zaidi ya watalii 59,000 walitembelea Bustani ya Shougang katika Eneo la Shijingshan mjini Beijing. Idadi hiyo ilikuwa mara 3.6 zaidi ya siku za kawaida -- ikionyesha hamu kubwa ya watu ya kusafiri.
Watu wakifurahia wakati wa tamasha la barafu na theluji katika Bustani ya Yuanmingyuan mjini Beijing, China, Desemba 31, 2022. (Xinhua/Luo Xiaoguang)
Uchumi wa barafu na theluji pia umefufuliwa kutokana na mabadiliko ya misimu. Beijing, mji ulioandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi mwaka jana, ilifungua viwanja vyote vitano vya barafu vya manispaa na maeneo ya mapumziko ya theluji wakati wa likizo ya siku tatu ya Mwaka Mpya.
Maeneo yenye vivutio vya kitalii ikiwemo Summer Palace, Bustani ya Beihai na Bustani ya Yuanmingyuan, yalianzisha shughuli za burudani kwenye barafu na theluji, ambazo zilivutia zaidi ya watalii 50,000 wakati wa likizo hiyo.
Watu wakiburudika kwenye uwanja wa barafu katika Bustani ya Beihai iliyoko Beijing, China, Desemba 31, 2022. (Xinhua/Chen Zhonghao)
Kando na bustani na maeneo yenye mandhari nzuri, maduka makubwa na mikahawa katika miji ya China pia ilijaa wanunuzi wa bidhaa na huduma.
Kamati ya Biashara ya Shanghai imejulisha kuwa, kuanzia Tarehe 23 Desemba 2022 hadi Januari 28, 2023, mji huo utaandaa zaidi ya shughuli 100 za kutangaza ununuaji wa bidhaa na huduma mbalimbali na kutoa idadi kubwa ya punguzo la bei kwa bidhaa.
Takwimu zilitolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zimeonesha kuwa, China ilirekodi takribani watalii milioni 52.7 wa ndani wakati wa likizo ya siku tatu ya Mwaka Mpya -- ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.44 kuliko mwaka uliopita.
Watu wakila chakula kwenye mkahawa mmoja hapa Beijing, China, Januari 1, 2023. (Xinhua/Ren Chao)
Takwimu hizo za wizara hiyo zimeonesha kuwa, mapato ya utalii yaliyopatikana katika likizo hiyo yalifikia zaidi ya yuan bilioni 26.5, ikiwa ni ongezeko la hadi asilimia 4 kuliko lile la kipindi kama hicho mwaka jana.
Takwimu hizo za Wizara hiyo pia zimeonesha kuwa, safari za kitalii za masafa mafupi zilipendelewa haswa na wasafiri katika kipindi hiki, na takwimu pia zinaonyesha kufufuka na kuanza kurejea kawaida kwa viwango vya usafiri wa masafa ya kati na marefu nchini China.
Wasafiri wakitoka kwenye Stesheni ya Reli ya Nanjing huko Nanjing, mji kuu wa Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Januari 2, 2023. (Picha na Su Yang/Xinhua)
Wateja wakienda kufanya manunuzi kwenye duka kubwa la Kunming, Mkoa wa Yunnan nchini China, Januari 1, 2023. (Picha na Liang Zhiqiang/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma