Lugha Nyingine
China yashuhudia safari milioni 52.7 za watalii wa ndani katika likizo ya Mwaka Mpya
Watalii wakijipiga picha za selfie kwenye Bustani ya Tiande huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong nchini China, Januari 1, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)
BEIJING - China imeshuhudia takribani safari milioni 52.7 za watalii wa ndani wakati wa likizo ya siku tatu ya Mwaka Mpya, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.44 kuliko mwaka jana , kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zilizotolewa siku ya Jumatatu.
Wizara hiyo imeeleza kuwa, mapato ya utalii yaliyopatikana katika likizo hiyo yamefikia zaidi ya yuan bilioni 26.5 (kama dola bilioni 3.8 za Kimarekani), ikiwa ni kiwango cha juu kwa asilimia 4 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.
Soko la utamaduni na utalii la China limeendelea kuwa tulivu na lenye utaratibu wakati wa likizo hiyo, ambayo imekamilika jana Jumatatu, imeongeza wizara hiyo katika taarifa yake.
Wizara hiyo imeeleza kuwa, safari za kitalii za masafa mafupi hupendelewa zaidi na wasafiri katika kipindi hicho, kukiwa na umaarufu unaoendelea kuongezeka wa shughuli za barafu na theluji, kupiga kambi, na michezo ya maingiliano kwa kuigiza kwenye mifumo ya kompyuta miongoni mwa vijana.
Wizara hiyo imesema takwimu hizo pia zinaonyesha ahueni ya kufufuka kwa safari za kitalii za umbali wa kati na mrefu nchini China, na baadhi ya mashirika ya usafiri mtandaoni yameripoti ongezeko kubwa la uwekaji oda za tiketi kwa utalii wa kuvuka mikoa na mipaka wakati wa likizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma