Lugha Nyingine
Mwaka 2022 katika Kumbukumbu: Mambo 10 Muhimu yaliyovutia hisia nchini China Mwaka 2022
Katika kurejea kumbukumbu za mambo mbalimbali muhimu ya Mwaka 2022, China imepata mafanikio mengi ya kupongezwa katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Uzalishaji wa nafaka wa China umekuwa mkubwa kwa miaka minane mfululizo, uzalishaji na mauzo ya magari yanayotumia nishati mbadala umefikia kiwango kipya, nyumba kongwe za miji zimepata sura mpya, mtandao wa 5G "unaunganisha tarafa na wilaya", na uchumi wa kidijitali unaendelea kuongoza Dunia...Hebu tuangalie mambo muhimu kupitia takwimu hizi kumi:
Uzalishaji wa nafaka wazidi kilogramu bilioni 650: nafaka yapata mavuno kwa miaka minane mfululizo nchini China
Picha hii inaonyesha wakulima wakikausha mahindi katika Mji Mdogo wa Anqing, eneo la Songshan, Mji wa Chifeng. (Picha na Li Fu, visual.people.cn)
Mwaka huu, maeneo yote ya China yalishinda kwa ufanisi changamoto ngumu kama vile mafuriko ya mvua kwenye Kaskazini na joto la juu linalodumu na ukame kwenye Kusini mwa China, na kupata ongezeko la uzalishaji wa nafaka kwa mwaka mzima. Mwaka 2022, uzalishaji wa jumla wa nafaka wa China umefikia kilogramu bilioni 686.53, na uzalishaji wa nafaka umebaki thabiti kwa zaidi ya kilogramu bilioni 650 kwa miaka minane mfululizo.
Mwaka huu, maeneo yote ya China yalishinda kwa ufanisi changamoto ngumu kama vile mafuriko ya mvua kwenye Kaskazini na joto la juu linalodumu na ukame kwenye Kusini mwa China, na kupata ongezeko la uzalishaji wa nafaka kwa mwaka mzima. Mwaka 2022, uzalishaji wa jumla wa nafaka wa China umefikia kilogramu bilioni 686.53, na uzalishaji wa nafaka umebaki thabiti kwa zaidi ya kilogramu bilioni 650 kwa miaka minane mfululizo.
Zaidi ya mizigo bilioni 100: Usafirishaji wa vifurushi na mizigo waonesha uhimilivu wa uchumi wa China
Tarehe 1, Desemba, jukwaa la takwimu la idara ya posta ya China lilionesha kuwa, mizigo iliyosafirishwa nchini China ya mwaka 2022 imezidi rasmi bilioni 100. Hali hiyo imetokea kwa siku 7 mapema kuliko mwaka jana.
Nchini China kumekuwa na mizigo na vifurushi bilioni 100 vya kusafirishwa kwa haraka Mwaka 2022, ikiwa ni wastani wa milioni 300 kwa siku, ambapo milioni 100 vimesafirishwa na kutolewa ndani na nje ya maeneo ya vijijini. Kwa sasa, sambamba na uboreshaji unaoendelea wa mfumo wa usafirishaji na miundombinu ya kibiashara, bidhaa zaidi na zaidi za viwandani zinaingia vijijini, na mazao mengi ya kilimo yanapita kwenye soko la kitaifa.
Nyumba 52,000 kongwe za miji yapata sura mpya
Picha hii inaonyesha mradi wa uhuishaji miji uliokamilika katika Mji Mdogo wa Xiakou, eneo la Nan'an la Chongqing, China. (Picha na Guo Xu, visual.people.cn)
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya China, kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, maeneo 52,100 ya makazi makongwe ya mijini yalijengwa upya nchini kote China, na familia milioni 8.5925 wamenufaishwa
Ujenzi wa kijani wachukua zaidi ya 90% ya majengo mapya
Kuanzia majengo ya kijani hadi vifaa vya ujenzi vya kijani, hadi maendeleo makubwa ya mbinuza ujenzi wa kijani, China imetimiza kikamilifu lengo la kuokoa matumizi ya nishati katika majengo mapya. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya China, hadi kufikia nusu ya kwanza ya Mwaka 2022, eneo jipya la ujenzi wa kijani nchini China lilikuwa zaidi ya 90% ya majengo mapya yote.
Kiwango cha pensheni kwa wastaafu kitaongezwa tena kwa 4%
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii na Idara nyinginezo, kuanzia Januari 1, 2022, pensheni ya msingi itaongezwa kwa wastaafu kutoka mashirika, wakala na taasisi za serikali ambao wamekamilisha taratibu za kustaafu kwa mujibu wa kanuni na kupokea pensheni za kimsingi za kila mwezi kufikia mwisho wa Mwaka 2021. Kiwango cha jumla cha marekebisho ni 4% ya pensheni ya msingi ya kila mwezi kwa wastaafu katika Mwaka 2021.
Zaidi ya magari milioni 6 yanayotumia nishati mpya yaundwa na kuuzwa
Karakana ya uundaji magari ya Kiwanda cha Magari cha Changan katika Mji wa Nanjing, Mkoa wa Jiangsu nchini China ni eneo lenye shughuli nyingi. Wafanyakazi hufanya kazi kwa muda wa ziada ili kuzalisha magari yanayotumia nishati mpya na kukidhi mahitaji ya oda za soko. (Picha na Zhu Hongsheng, visual.people.cn)
Katika miaka ya hivi karibuni, magari ya BYD, Weilai na magari mengine yanayotumia nishati mpya yamefanikiwa kutua Ujerumani, Uholanzi, Sweden, Denmark na maeneo mengine, na chapa zinazomilikiwa kwa kujitegemea na makampuni ya China zimepata mafanikio makubwa katika mauzo kwenye masoko ya nje kama Ulaya, Marekani na masoko mengine.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Waundaji Magari la China, kuanzia Januari hadi Novemba 2022, uzalishaji na mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya ulifikia magari milioni 6.253 na milioni 6.067 mtawalia, na hivyo kuongezeka maradufu mwaka hadi mwaka.
Viwanda maalum vidogo na vya kati (SMEs) vya teknolojia ya hali ya juu karibia 9000 vyastawi vizuri
Wafanyakazi wakizalisha nyenzo za betri za lithiamu katika karakana ya mradi wa utengenezaji bidhaa kwa kutumia akili bandia rafiki kwa mazingira katika kiiwanda maalumu kidogo na cha kati cha teknolojia ya hali ya juu katika mji mdogo wa Longnan, Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi, Desemba 24, (Picha na Zhu Haipeng, visual.people.cn)
Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya msukumo wa mfululizo wa hatua za kisera, maendeleo ya viwanda maalumu vidogo na vya kati (SMEs) vya teknolojia ya hali ya juu vya China yameendelea kukua. Kwa kuchukua mfano wa viwanda maalum vidogo na vya kati maarufu kama “viwanda vipya maalum vidogo vyenye mchango mkubwa”, tangu Juni 2019, kundi la kwanza la makampuni 248 limetambuliwa, na hadi sasa, jumla ya makampuni 8,997 yametambuliwa katika makundi 4, yakiwa na wastani wa hataza na hakimilki za uvumbuzi 15.7 zinazomilikiwa na kila kampuni. Viwanda maalumu vipya vidogo na vya kati vya teknolojia ya hali ya juu vimekuwa msingi muhimu kwa maendeleo ya hali ya juu ya tasnia ya utengenezaji bidhaa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
Vituo zaidi ya milioni 2.2 vya Mtandao wa 5G vyafunguliwa “wilaya hadi wilaya"
Wafanyakazi wakijaribu antena kwenye mnara wa kituo cha 5G katika Tarafa ya Xuba, Eneo la Yi'an, Mji wa Tongling, Mkoa wa Anhui, China. (Picha na Guo Shining, visual.people.cn)
Hivi karibuni, "Waraka kuhusu Maendeleo ya China ya Mtandao wa Intaneti 2022" uliotolewa na Taasisi Kuu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya China, unaonesha kuwa China imejenga mtandao wa 5G ulio mkubwa zaidi na wa teknolojia ya juu zaidi duniani. Kwa msingi huu, huduma hiyo inaenea zaidi kwenye miji midogo na wilaya zote, baada ya kuenea kwenye miji kote nchini.
Uwezo wa uzalishaji wa nishati mbadala waongezeka na kufikia kilowati zaidi ya milioni 100
Wafanyakazi wakitekeleza ufungaji wa mwisho wa moduli katika eneo la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua unaoelea kwenye maji wa hifadhi ya maji inayozunguka ya Tawi la Operesheni za Uzalishaji Umeme la Liaocheng la Shirika la Taifa la Nishati la Shandong Electric Power (Picha na Zhang Zhenxiang, visual.people.cn)
Takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Novemba 2022, uwezo wa kuzalisha nishati mbadala wa mitambo mipya iliyofungwa nchini China umefikia kilowati milioni 113.69, na uzalishaji wa umeme utaendeleza mwelekeo wa maendeleo ya kijani.
Kasi ya uchumi wa kidijitali wa China yazidi kuongezeka kwa kufikia dola za Kimarekani Trilioni 7.1
Waraka wa "Uchumi wa Kidijitali Duniani Mwaka (2022)"uliotolewa hivi karibuni na Taasisi Kuu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya China unaonyesha kuwa Mwaka 2021, kiwango cha uchumi wa kidijitali wa China kilikuwa dola za kimarekani trilioni 7.1, ikishika nafasi ya pili duniani. Kwa sasa, mtandao wa kiviwanda umeunganishwa kikamilifu katika nyanja kubwa 45 za uchumi wa taifa, na kiwango cha viwanda kimepita alama ya kiasi cha thamani ya yuan trilioni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma