Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping na mwenzake wa Benin watumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa tena kwa uhusiano wa kidiplomasia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Alhamisi alitumiana salamu za pongezi na Rais wa Benin Patrice Talon kwa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa tena kwa uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema katika kipindi cha nusu karne tangu kuanzishwa tena kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Benin, nchi hizo mbili zimekuwa zikitendeana kwa dhati na kwa urafiki, na kuunga mkono kithabiti masuala yanayohusu masilahi ya msingi ya kila upande na mambo muhimu yanayofuatiliwa nazo.
Rais Xi amesema, hivi sasa uhusiano wa nchi hizo mbili unadumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo na matokeo ya ushirikiano wenye matunda mazuri katika nyanja mbalimbali, ambayo yameleta manufaa yanayoonekana kwa watu wao.
Rais Xi amesema anathamini maendeleo ya uhusiano kati ya China na Benin na yuko tayari kushirikiana na Rais Talon ili kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali kwenye ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ili kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufikia kiwango kipya.
Kwa upande wake, Talon amesema ameridhishwa na ushirikiano wenye tija kati ya nchi hizo mbili tangu kurejeshwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita.
Talon ameongeza kuwa yuko tayari kushirikiana na Rais Xi ili kujenga uhusiano thabiti na wenye nguvu zaidi baina ya nchi hizo mbili, akieleza imani yake kwamba ushirikiano usioweza kuvunjika wa Benin na China hakika utapata matokeo makubwa zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma