Lugha Nyingine
China yatekeleza mbinu mbalimbali ili kuvuka hali ngumu ya kiuchumi Mwaka 2022
Picha iliyopigwa Oktoba 19, 2020 ikionyesha mwonekano wa nje wa Benki ya Umma ya China katika Mji wa Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)
BEIJING - China, nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, imepita safari isiyo ya kawaida Mwaka 2022, mwaka ambao umekuwa na "mambo yasiyotarajiwa" ambayo yalijaribu uwezo wa watunga sera na watoa maamuzi ya usimamizi wa uchumi mkuu.
Milipuko ya virusi vya Korona hapa na pale nchini China na migogoro inayotokana na siasa za kijiografia katika sehemu nyingine za Dunia kwa pamoja vimetatiza mwelekeo wa ukuaji wa uchumi wa China.
Uchumi wa China ulianza vyema kwa kupanuka kwa asilimia 4.8 katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022. Pato lake la Taifa lilishuka hadi asilimia 0.4 katika robo ya pili na kuongezeka hadi asilimia 3.9 katika robo ya tatu.
Kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika robo hiyo ya pili, kulisababisha mwitikio wa haraka wa serikali, na mfululizo wa sera na hatua za ufuatiliaji zilitekelezwa ili kudumisha utulivu wa jumla wa kiuchumi.
Hakuna kuanzisha vichocheo vya kiuchumi “kama mafuriko”
Tofauti na uchumi wa nchi nyingi duniani zilizoamua kurahisisha sera za fedha ili kuchochea ukuaji, China imejiepusha na kuanzisha vichocheo vikubwa, ili kuepuka kuathiri maslahi ya muda mrefu.
Benki kuu ya China ilisisitiza "hakuna vichocheo kama mafuriko" katika ripoti zake tatu za utekelezaji wa sera za robo mwaka, na kutuma ishara wazi ya azma yake ya kuambatana na msimamo wa busara wa sera ya fedha.
"Kwa kuzingatia operesheni ya kiuchumi, sera kuu za China zimetekelezwa ipasavyo," alisema mkuu wa Benki ya Umma ya China (PBOC), Yi Gang.
"Dumisha milima ya kijani"
Jumuiya kubwa ya wadau wa soko wa China, zaidi ya milioni 160 kwa jumla, ndio wapokeaji wakuu wa sera mahsusi za China.
Mbali na usaidizi wa mikopo uliowekwa maalum, Serikali ya China imeanzisha upunguzaji wa kodi, tozo na ada mbalimbali ili kupunguza mzigo wa kifedha kwa biashara, ambazo -- mara nyingi hujulikana kama "milima ya kijani" kutokana na jukumu lake la msingi katika kuchochea upanuzi wa kiuchumi – zibaki zikiwa na ukwasi.
Marejesho ya mikopo ya kodi ya nyongeza za thamani nchini China yalifikia karibu yuan trilioni 2.4 (kama dola za Marekani bilioni 344.43), ikiwa ni rekodi ya juu na zaidi ya mara 3.5 ya kiasi cha mwaka jana.
Kutembea katika njia sahihi
Mwezi Aprili, mwaka huu uongozi wa China ulipendekeza kwamba nchi hiyo lazima idhibiti janga la UVIKO-19, kuleta utulivu wa uchumi na kuweka maendeleo kwenye njia sahihi.
"Inajumuisha nadharia ya kimfumo ya kupata usawa wa nguvu kati ya malengo mengi," amesema Liu Shangxi, Mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya Mambo ya Fedha ya China.
Milipuko ya UVIKO-19 na sekta ya kupoeza ya mali isiyohamishika ni miongoni mwa mambo makuu yanayoathiri uchumi wa China mwaka huu, na serikali imeweka sera za kurekebisha vizuri ili kupunguza athari zao huku ikijilinda dhidi ya hatari zinazoweza kutokea.
"Uratibu wa sera utaimarishwa ili kuunda harambee kwa ajili ya maendeleo ya hali ya juu Mwaka 2023," uongozi wa China ulisema kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kazi ya uchumi uliofanyika katikati ya Desemba.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma