Lugha Nyingine
Uchumi wa China kuendelea kusukuma uchumi wa Dunia kufufuka na kukua Mwaka 2023
Meli ikiwa imepakia magari yanayotumia nishati ya umeme ya kampuni ya kuunda magari ya Tesla kutoka Marekani kwenye kiwanda cha Shanghai nchini China, kabla ya kuondoka kuelekea Slovenia kutoka Bandari ya Shanghai, Mashariki mwa China, Mei 11, 2022. (Xinhua)
BEIJING - Mwaka 2022 umeshuhudia uchumi wa Dunia ukiyumba kutokana na mshtuko uliotokana na msururu wa mambo yasiyojulikana. Na Mwaka 2023 unaweza kuwa mwanzo mbaya kwa sababu ya athari zinazoendelea za matukio kama vile vita kati ya Ukraine na Russia, kuongezeka kwa viwango vya riba kunakotekelezwa na Benki Kuu ya Marekani, mfumuko wa bei duniani, matatizo ya nishati na chakula, na pia janga la virusi vya Korona ambalo bado linaendelea.
Kutokana na hali ya kutatanisha ya mazingira ya kimataifa, China imedumisha misingi mizuri na kutafuta maendeleo ya hali ya juu. Uthabiti na uwezo wa uchumi wake umetia matumaini kwenye imani ya jumuiya ya kimataifa katika kuufanya uchumi wa Dunia Mwaka 2023 kufufuka na kukua.
"Dunia yenye matatizo mengi"
Watu wa kawaida duniani kote tayari wamekuwa wakiishi maisha magumu Mwaka 2022: kukodisha nyumba ni ghali sana, bili ya nishati ni kubwa sana kumudu, kwenda kwenye maduka makubwa mara nyingi kunamaanisha kutazama tu mboga za majani zinazouzwa.
"Huenda tunaingia katika zama mpya ya Mdororo Mkubwa Usiodhibitika," Nouriel Roubini, profesa mstaafu wa uchumi na biashara ya kimataifa katika Chuo cha Biashara katika Chuo Kikuu cha New York, aliandika kwenye makala ya gazeti la Time Mwezi Oktoba.
"Tunapitia mabadiliko ya kimsingi katika uchumi wa Dunia kutoka kutabirika ... hadi Dunia iliyo na udhaifu zaidi," Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Kristalina Georgieva alisema mapema Oktoba.
Mteja akichagua nguo katika duka huko Queens, New York, Marekani Tarehe 23 Desemba 2022. (Picha na Ziyu Julian Zhu/Xinhua)
Hatua ya mgawanyiko
IMF tayari imepunguza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa Dunia Mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 Mwezi Oktoba. Hata hivyo, Georgieva amesisitiza tena katikati ya Desemba kwamba uwezekano wa kushuka zaidi katika makadirio yake utakuwa "juu," akiuita Mwaka 2023 "mwaka mgumu sana."
Wakati huo huo, wafuatiliaji wengi wa uchumi duniani wanaamini kuwa Mwaka 2023 unaweza kuwa na hatua mgawanyiko, na nchi zilizoendelea zinaweza kutumbukia kwenye mdororo na uchumi unaoinukia kuanza kuimarika huku nchi zinazoendelea hususan za Asia Mashariki na China zikichochea kufufuka na kukua kwa uchumi wa duniani.
Kiatipong Ariyapruchya, mwanauchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia Tawi la Thailand amesema, Asia Mashariki itadumisha ukuaji mkubwa wa uchumi Mwaka 2023, na kuimarika kwa uchumi wa China kutatumika kama "mwinuko" wa kufufua uchumi wa Dunia.
Mchumi mkuu wa IMF Pierre-Olivier Gourinchas (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 11, 2022. (Xinhua/Liu Jie)
Kuvuka giza
Katika kukabiliwa na kuongezwa kwa migogoro Mwaka 2022, China imedumisha utulivu wa jumla wa uchumi wake kwa kuratibu ipasavyo sera za UVIKO-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuanzisha sera mfululizo za vichocheo kusaidia biashara, kuleta utulivu wa bei za wanunuzi bidhaa, na kuongeza imani ya wawekezaji wa kimataifa.
Fukaishi Akihiro, Mkuu wa Kampuni ya Epson (China) anasema kuwa chini ya janga hili, kampuni bado inaona ukuaji wa biashara na maendeleo nchini China.
Watu wakichagua vyakula katika kituo cha biashara kilichoko Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 25, 2022. (Xinhua/Zhang Chenlin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma