久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Wajasiriamali wa China wahamasishwa kwenda nje kutafuta fursa za biasahra

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2022

Shughuli ya mafunzo ikifanyika ili kujiandaa kabla ya wajasiriamali wa makampuni ya China kuanza safari zao za ng'ambo kutafuta fursa za biashara kwa usaidizi wa serikali, huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, Desemba 14, 2022. (Xinhua)

HEFEI - Shughuli ya mafunzo imefanyika siku ya Jumatano huko Hefei, Mji Mkuu wa Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kabla ya wajasiriamali wa makampuni ya China kuanza safari zao za ng'ambo kutafuta fursa za biashara chini ya usaidizi wa serikali.

Kwa mujibu wa Idara ya Biashara ya Mkoa wa Anhui, watu 119 kutoka makampuni 54 watafanya safari zao za kibiashara ng'ambo kutembelea wateja watarajiwa na kutafuta ushirikiano kuanzia Jumatano hadi mwisho wa mwaka huu.

Idara hiyo pia itatumia ndege maalumu ya kukodi kutuma ujumbe wa wafanyabiashara na wajumbe kutoka zaidi ya makampuni 50 ya mkoa huo kwenda Japani na Jamhuri ya Korea (ROK) Desemba 25, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Mkoa wa Anhui kupanua soko lake la ng'ambo na kukuza biashara ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Liu Guang, ambaye ni naibu mkurugenzi wa idara ya biashara ya Anhui, shughuli zote ziko chini ya kampeni ya kuhimiza biashara ya mkoa huo, inayolenga kuvutia oda zaidi za biashara na uwekezaji wa kigeni. Ukiacha kando maonyesho ya mtandaoni na nje ya mtandao, Anhui pia itaandaa zaidi ya shughuli 100 za kuhimiza uwekezaji nje ya nchi Mwaka 2023 ili kuleta miradi mikubwa ya uwekezaji wa kigeni.

"Tutaandaa shughuli maalum za kujitangaza katika nchi na maeneo ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Uingereza, na Korea Kusini, ambapo wajasiriamali wetu wanaweza kuwasiliana na kushirikiana na makampuni ya biashara kutoka kwenye tasnia mbalimbali ikiwa ni pamoja na magari yanayotumia nishati mpya, vifaa vya kisasa vya majumbani, na semiconductors," amesema Liu.

Tangu China itangaze sera mpya ya hatua za kukabiliana na UVIKO-19, idara ya biashara ya Anhui imetuma watu 58 kutoka makampuni 18 kushiriki kwenye shughuli, ikiwa ni pamoja na maonyesho na mazungumzo ya biashara katika nchi 19. Na juhudi hizo za pamoja zimezaa matunda katika kazi za sekta mbalimbali, kutoka kwenye maendeleo ya nyenzo na utafiti, bioteknolojia, ujenzi, na utengenezaji wa bidhaa, hadi biashara ya jumla na rejareja.

Chen Xiaojun, mwenyekiti wa Kampuni ya Nuntius Bonded Logistics Center (Anhui), na msaidizi wake, Shen Tubo, wamekuwa kwenye pilika za safari zao zenye shughuli nyingi barani Ulaya tangu Tarehe 8 Desemba.

"Tumezungumza kuhusu biashara ikiwa ni pamoja na biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka, uanzishwaji wa maghala nje ya nchi, na oda za masanduku na washirika kadhaa katika nchi zikiwemo Ubelgiji na Uholanzi. Tunapiga hatua chanya katika ushirikiano," amesema Chen.

Chen Xiaojun, Mwenyekiti wa Kampuni ya Nuntius Bonded Logistics Center (Anhui), akiwa kwenye mkutano na wateja nchini Ubelgiji, Desemba 10, 2022. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>