Lugha Nyingine
Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji duniani wa Shenzhen 2022 wahusisha uwekezaji wa Yuan bilioni 879
(Picha ilitolewa na mwandalizi.)
Tarehe 9, Desemba, mkutano wa kuvutia uwekezaji duniani wa Shenzhen 2022 ulifanyika kwenye Hoteli ya Wuzhou, ambapo makubaliano ya miradi 315 yalitiwa saini au kujadiliwa, na thamani ya jumla ya uwekezaji ilifikia Yuan bilioni 879.
Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China Siddharth Chatterjee na watu wengine walitoa pongezi kwa mkutano huo. Katibu wa Kamati ya Chama ya Shenzhen Meng Fanli alishiriki na kutoa hotuba kwenye mkutano.
Kwa jumla makubaliano ya miradi 48 yalitiwa saini pamoja, yakihusu miradi na kampuni za Amazon, Intel, Hexagon na kampuni nyingine, katika sekta mbalimbali kama vile teknolojia mpya ya habari na ektroniki, matibabu na dawa za kiviumbe na afya, mambo ya fedha n.k.
Mazingira mazuri ya kufanya biashara ya Shenzhen yamerutubisha maendeleo ya makampuni. Katika mkutano huo, mshiriki wa PricewaterhouseCoopers (PwC) ambaye ni mwezi wa msimamizi wa uchumi kwenye eneo la China Zhang Lijun alisema, baada ya maendeleo ya zaidi ya miaka 40 , mji wa Shenzhen umekuwa “mfano wa kuigwa wa mafanikio” miongoni mwa maeneo maalumu ya kiuchumi zaidi ya 4,000 duniani kote. “Hivi sasa mji wa Shenzhen umepata fursa ya kihistoria ya maendeleo, ukiwa kituo kisichokosekana kwa makampuni ya nchi za nje kuwekeza nchini China.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma