Lugha Nyingine
Shirikisho la Biashara la Makundi ya Wafanyabiashara Wateochew ya Bandari Huria ya Kimataifa laanzishwa Hainan
Shirikisho la Biashara la Makundi ya Wafanyabiashara Wateochew ya Bandari Huria ya Duniani lilianzishwa Hainan.
Tarehe 4 Desemba, Shirikisho la Biashara la Makundi ya Wanyabiashara Wateochew ya Bandari Huria ya Duniani lililoanzishwa na mashirikisho maarufu ya wafanyabiashara wateochew, kama vile shirika la uhimizaji wa uchumi wa wafanyabiashara wateochew la Hainan, shirikisho la wafanyabiashara wateochew wa Umoja wa Falme za Kiarabu, shirikisho la wateochew la Ufaransa, shirikisho la wafanyabiashara wateochew la Marekani, shirikisho la wafanyabiashara wateochew la Canada, limetia saini kwenye pendekezo la "Makubaliano ya Hainan" kwenye Mkutano wa 21 wa Makundi ya Ushirikiano wa Kichumi ya Wanyabiashara Wateochew wa Kimataifa.
Shirikisho hilo linalenga kuhimiza ushirikiano kati ya wafanyabiashara wateochew nchini na nje ya nchi, kufuata msingi wa nafasi ya kimkakati ya Bandari Huria ya Hainan, kutumia vya kutosha nguvu bora ya rasilimali za bandari kuu tano za biashara huria, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kufuata hali halisi kati ya bandari kuu za biashara huria katika mitaji, wataalamu, teknolojia, takwimu na nyanja nyingine, pamoja na kuhimiza maendeleo ya bandari huria mpya duniani, kutegemea soko kubwa la matumizi la China ili kuunda muundo wa kunufaika pamoja na rasilimali za biashara huria duniani.
Katika siku za baadaye, shirikisho hilo litahamasisha na kuwashirikisha wafanyabiashara wateochew wa bandari huria duniani kufanya mawasiliano ya kiuchumi na ushirikiano katika viwanda, kuhimiza mawasiliano na kunufaika pamoja na mtaji, teknolojia, wataalamu na takwimu, na kufanya shughuli za mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara na ukaguzi wa biashara kila baada ya muda uliowekwa, na kuongeza maoni ya pamoja kuhusu makubaliano ya Hainan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma