Lugha Nyingine
Mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la“Ukanda Mmoja, Njia Moja”na Mkutano wa Makundi ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Wafanyabiashara Wateochew wa Kimataifa Wafanyika Hainan
Mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Ngazi ya Juu la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”na Mkutano wa Makundi ya Ushirikiano wa Kichumi ya Wanyabiashara Wateochew wa Kimataifa kwenye eneo la biasahra huria imefunguliwa Desemba 4 huko Boao, mkoani Hainan, China. Wakati wa mikutano hiyo, wanasiasa na wafanyabiashara wanaotoka nchini na nje wamejadili mada kuhusu “Kutekeleza pendekezo la Maendeleo ya Dunia, na kuhimiza maendeleo endelevu ya kijani”, wakitafuta kwa pamoja njia bora zaidi za kutimiza lengo la maendeleo endelevu, kutoa maoni yao yenye busara kuhusu mpango wa China wa kuboresha usimamizi wa mazingira ya dunia, kuharakisha muundo wa uchumi wa kutoa kabo chache, ili kutimiza ufufukaji na maendeleo ya uchumi. Mikutano hiyo ni moja ya shughuli za Mkutano wa mwaka wa 21 wa Makundi ya wateochw wa Kimatiafa.
Waziri mkuu wa Cambodia Hun Sen, Rais wa Philippine Marcos na Waziri wa mambo ya ndani wa Philippine Benjamin wametuma salamu za pongezi kwa Shirikisho kuu la Makundi ya Wateochew ya Kimataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Wafanyabiashara Wateochew wa Kimataifa, wakisifu sana pendekezo la maendeleo ya dunia, na kuunga mkono wateochew na wafanyabiashara wachina wanaoishi sehemu mbalimbali duniani katika kutekeleza kwa pamoja pendekezo la maendeleo ya dunia, na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya kijani.
Naibu waziri mkuu wa Thailand Wai Sanu alisema kwenye barua yake ya pongezi kuwa, mikutano hiyo ya Hainan inafuatilia pendekezo la maendeleo ya dunia na maendeleo endelevu ya kijani, inafanyika katika wakati wa kufaa, angependa kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya wafanyabiashara wateochew, Mkoa wa Hainan na nchi ya Thailand katika sekta mbalimbali.
Waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa Myanmar Angkor Golai, mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China Chang Qide na ofisa wa shirika husika la Umoja wa Mataifa Li Nan wametoa hotuba kwa njia ya video.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Hainan Miao Yanhong amesema, hivi sasa Mkoa wa Hainan unahamasisha watu wote wa mkoa mzima kuhimiza kazi ya bandari ya biashara huria ianze mapema, kuharakisha kufanya mafungamano ya kimataifa, kuboresha mazingira ya uendeshaji wa biashara, na kuwavutia kwa nguvu kubwa wafanyabishara wa kote duniani, kazi mbalimbali zinaendelea vizuri na kupata ufanisi dhahiri. Mkoa wa Haina unatarajia kwa udhati Shirikisho kuu la Makundi ya Wateochw wa Kimataifa na Jumuiiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya wafanyabiashara wateochw wa kimataifa vifanye kazi kama daraja, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, na kuhimiza pande mbalimbali zipate maendeleo kwa pamoja.
Mwenyekiti wa Shirikisho kuu la Makundi ya Wateochew wa Kimataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa mwaka wa 21 wa shirikisho hilo Hong Jiangyuo alisema kuwa, Mkoa wa Hainan ukiwa bandari kubwa zaidi ya biashara huria duniani, umefanya kazi kubwa sana katika ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Wanatarajia Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya wafanyabiashara wateochew wa kimataifa itachukua fursa ya mkutano wa mwaka kuwaongoza wafanyabiashara wateochew wanaoishi sehemu mbalimbali duniani katika kukusanya maoni mamoja, kuimarisha ushirikiano, kunufaika pamoja na raslimali, na kutekeleza kivitendo pendekezo la maendeleo ya dunia, ili wawe washiriki muhimu wa ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia, na kujenga pamoja siku nzuri za binadamu za baadaye.
Mkuu wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya wafanyabiashara wateochew wa kimataifa Wu Kaisong, mjumbe wa kudumu wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la kitaifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya wasimamizi ya Shirikisho kuu la wafanyabiashara la ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” Lin Jianyue, mshauri wa heshima wa Baraza la juu la Bunge la Taifa la Thelend na wengineo, wametoa hotuba kwenye mikutano hiyo kuhusu kutekeleza pendekezo la maendeleo ya dunia na kuhimiza maendeleo endelevu ya kijani.
Wakati wa kufanyika kwa mikutano hiyo, pia zilifanyika hafla za kusaini makubaliano kuhusu miradi ya Kituo cha uzalishaji, mafunzo na utafiti wa dawa za kitaifa za watoto, na biashara ya bidhaa kwenye eneo la ushuru wenye nafuu la Yangpu. Mikutano hiyo pia ilitoa taarifa ya pamoja ya “kutekeleza pendekezo la maendeleo ya dunia, na kuhimiza maendeleo endelevu ya kijani”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma