Lugha Nyingine
EAC kuanzisha mradi wa kuboresha biashara ya kikanda ya mbegu za viazi
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imekabidhi vifaa vya maabara kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, kama sehemu ya mradi unaolenga kuboresha biashara ya kikanda ya mbegu za viazi.
Katika taarifa yake iliyoitoa jana Jumanne, EAC imesema mradi huo unalenga kutoa mazingira ya kuendeleza biashara ya mbegu za viazi kupitia kusaidia kuandaa mikakati ya kikanda na mipango kazi pamoja na kuendeleza na kuoanisha viwango vya mbegu za viazi vya kikanda.
Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki, amesema vifaa hivyo vya maabara vinatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika biashara ya mbegu za viazi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo, hasa katika kuimarisha uwezo wa kiufundi na kiutekelezaji wa watumishi na maabara kufanyia kazi ipasavyo hatua zinazohitajika za usafi na uhifadhi wa mimea (SPS) ili kuwezesha biashara ya mbegu za viazi katika kanda.
Mathuki ametilia mkazo kwamba vifaa hivi vya maabara vitaongeza uzalishaji, upatikanaji, ufanisi na uhakika wa mbegu za viazi zilizothibitishwa na zenye uhakika kwa uzalishaji na biashara katika kanda hii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma