Lugha Nyingine
Ukuaji wa GDP ya Marekani katika Robo ya Tatu ya Mwaka warekebishwa kwenda juu huku kukiwa na hofu ya kudorora kwa uchumi
Watu wakitembelea onyesho la "RE+ 2022" lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Anaheim huko Orange, California, Marekani Septemba 21, 2022. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)
WASHINGTON - Uchumi wa Marekani ulikua kwa kasi katika robo ya tatu ya mwaka kuliko makadirio ya awali yalivyoonyesha, lakini nchi hiyo bado inakabiliwa na uwezekano wa kudorora kwa uchumi mwaka ujao.
Pato la Taifa (GDP) -- thamani ya jumla ya bidhaa na huduma zote za Marekani -- lilipanda kwa asilimia 2.9 kwa kiwango cha mwaka, kwa mujibu wa makadirio ya pili yaliyotolewa Jumatano.
Kiwango hicho kimerekebishwa kutoka kwenye ongezeko la asilimia 2.6 lililoripotiwa mwezi uliopita.
Marekebisho hayo yameakisi ongezeko la matumizi ya biashara na ununuzi bidhaa na kupungua kwa uagizaji bidhaa kutoka nje.
Wakati huo huo, uchumi unakabiliwa na uwezekano wa kudorora katika nusu ya kwanza ya mwaka ujao, kwani Benki Kuu ya Marekani inajishughulisha na mzunguko wa ongezeko kubwa la viwango vya riba katika miongo minne, katika nia yake ya kumaliza mfumuko mbaya zaidi wa bei kuwahi kutokea tangu miaka ya 1980.
Utumizi mbaya wa fedha wa utawala wa sasa ndiyo wa kulaumiwa kwa kuwepo mfumuko wa bei uliokithiri, kwa mujibu wa wachumi.
Ishara kadhaa zinaonyesha uwezekano wa kushuka kwa uchumi mwaka ujao. Soko la nyumba linapungua, kwani ongezeko la viwango vya riba limetafsiri viwango vya juu zaidi vya rehani ambavyo havijawahi kutokea katika miaka 20 iliyopita, na kufanya iwe vigumu kwa wanunuzi kununua nyumba.
Kiwango cha rehani kisichosogea cha miaka 30 kilizidi kiasi cha asilimia 7 Mwezi Oktoba mwaka huu kwa mara ya kwanza katika miongo miwili, kwa mujibu wa data kutoka Taasisi ya Freddie Mac, ambayo inafadhili rehani.
Hiyo ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa asilimia 3.10 katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Aidha, uwekezaji kwenye makazi umepungua kwa robo sita za mwaka mfululizo.
Hata hivyo, uwezekano mzuri wa fedha unaofunika makadirio yoyote mabaya ya kiuchumi ni kwamba mtikisiko wowote wa uchumi unatarajiwa kuwa mfupi. Hiyo ni kwa sababu ya nguvu ya rekodi katika soko la nguvukazi la Marekani, wachumi wamesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma