Lugha Nyingine
Hunan, China yaagiza kambakoche hai kutoka Kenya
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022
Ndege iliyobeba kambakoche hai wa kilo 404 kutoka Nairobi ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Huanghua wa Mji wa Changsha siku ya Alhamisi iliyopita, likiwa ni shehena ya kwanza ya kambakoche iliyosafirishwa kutoka Kenya hadi Mkoa wa Hunan wa China mwaka huu.
Baada ya kukaguliwa katika Forodha ya Changsha, kambakoche hai hao wataingia kwenye soko la China.
Mfanyabiashara wa China wa uagizaji wa bidhaa alisema kuwa kambakoche wa Kenya ni wa bei nafuu kuliko kambakoche wa Australia. Anapanga kupanua uagizaji wake ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa China.
Forodha ya China imefungua njia ya kipaumbele ya kupita forodha kwa haraka kwa uajizaji wa aina za samaki hai kutoka nje.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma