久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Naibu Spika wa Bunge la Seneti la Ufaransa asema muundo wa maendeleo ya kisasa ya China unaendana na uhalisia wa mazingira yake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2022

Mfanyakazi akifanya kazi katika kampuni ya kuunganisha sehemu za magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) kwenye kiwanda cha Chery Holding Group katika Mji wa Wuhu, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, Oktoba 12, 2022. (Xinhua/Zhou Mu)

PARIS - Njia ya China ya kuelekea maendeleo ya kisasa, ni muundo wa maendeleo uliochukuliwa kulingana na hali halisi ya China, ni "muhimu na lazima iheshimiwe," Pierre Laurent, Naibu Spika wa Bunge la Seneti la Ufaransa amesema.

Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ni "muhimu sana" siyo tu kwa China na watu wa China, bali pia kwa Dunia nzima, kwani China imechukua nafasi kubwa katika jumuiya ya kimataifa baada ya miongo kadhaa ya maendeleo, amesema Laurent, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Chama cha Kikomunisti cha Ufaransa, katika mahojiano ya hivi majuzi na Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kati ya juhudi ambazo jumuiya ya binadamu imefanya, China imeweza kutafuta njia mpya inayofaa kwa hali yake yenyewe, Laurent amesema, huku akiongeza kuwa chaguo hili la kisiasa "limezaa matunda yake" kwa kuleta sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na kisha jitihada za kuharakisha maendeleo ya nchi.

Wakati wa uongozi wake akiwa katibu wa taifa wa chama chake kati ya Mwaka 2010 na 2018, Laurent alifanya ziara mara mbili nchini China, Mwaka 2011 na 2016 na alifurahishwa sana na maendeleo ya kushangaza ambayo China imepata ndani ya miaka mitano.

"Katika muongo mmoja uliopita, kinachoonekana wazi unapotembelea China ni njia (China) iliyosafiri ili kuiondoa nchi katika umaskini, na kujiweka kwenye njia ya maendeleo kwa kutimiza malengo yaliyowekwa ya kuifanya nchi hiyo kuwa yenye ustawi wa jamii, kama viongozi wa China na Chama cha Kikomunisti cha China wanavyotangaza," Laurent amesema.

Picha hii iliyopigwa kutokea angani ikionyesha mwonekano wa Bandari ya Kontena ya Kimataifa ya Yangpu katika Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi la Yangpu, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Mei 26, 2021. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Akizungumzia mipango ya Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping ya kuhimiza amani na maendeleo duniani na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, Laurent amesema kuwa Ufaransa na nchi nyingine duniani pia zinaweza kuchukua hatua ili kuendeleza mipango hiyo.

Changamoto kubwa za kimataifa kama vile usalama wa chakula na nishati na maendeleo ya kijamii "lazima zitatuliwe kupitia ushirikiano wa pande nyingi na kwa kuheshimu mataifa yote," Laurent amesisitiza.

“China itachukua nafasi kubwa katika harakati za kimataifa zinazoruhusu maendeleo ya wote,” ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>