Lugha Nyingine
Rais Ruto wa Kenya na katibu mkuu wa chama tawala cha UDA wampongeza Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC
Kiongozi wa chama tawala cha Kenya UDA ambaye pia ni Rais wa Kenya William Ruto ametuma barua ya kumpongeza Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC.
Kwenye barua yake, Rais Ruto kwa niaba ya watu wa Kenya na yeye mwenyewe, amesema Xi amekuwa mfano wa kuigwa kwa kuyapa kipaumbele maslahi ya wananchi na moyo wa kujitolea. Amesema, Kenya inatarajia kushirikiana na China katika kujenga jumuiya ya Afrika na China yenye mustakabali wa pamoja na iliyo na uhai.
Naye katibu mkuu wa chama cha UDA Bibi Veronica Maina pia ametuma barua ya pongezi kwa Xi Jinping akisema, chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPC na katibu mkuu wake Xi Jinping, China imepata mafanikio makubwa yanayoshangaza dunia nzima. Anaamini kuwa mawasiliano kati ya vyama hivyo viwili yataweza kuendelea kuhimiza uhusiano kati ya nchi mbili kuendelea vizuri kwa utulivu, na kutoa mchango katika kujenga jumuiya ya Afrika na China yenye mustakabali wa pamoja na yenye kiwango cha juu katika zama mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma