久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Uchumi wa China waonesha kuimarika kufuatia kupanuka katika robo ya tatu ya mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2022

(Picha inatoka Xinhua.)

BEIJING - Uchumi wa China umeonesha kuwa thabiti zaidi katika robo ya tatu ya mwaka huu huku viashiria vikubwa vikionyesha dalili chanya za utulivu, ukisaidiwa na juhudi za China kusawazisha udhibiti wa janga la UVIKO-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zimeonesha Jumatatu kuwa, Pato la Taifa la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 3.9 mwaka hadi mwaka na kufikia yuan trilioni 30.76 (kama dola trilioni 4.32 za Kimarekani) katika robo ya tatu ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.5 zaidi ya ile ya robo ya pili ya mwaka.

Kwa mujibu wa NBS, katika robo tatu za kwanza, Pato la Taifa liliongezeka kwa asilimia 3 kuliko lile la kipindi hiki cha mwaka jana , ikiwa ni asilimia 0.5 kwa kasi zaidi kuliko ile ya nusu ya kwanza ya Mwaka 2022.

“Viashiria vingi vikubwa vya uchumi vimeshuhudia maboresho makubwa ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika robo ya pili, huku mahitaji ya viwanda vya kuzalisha bidhaa yakiimarika taratibu, na bei na ajira zikibaki kuwa tulivu,” NBS imesema katika taarifa yake.

Uchanganuzi wa takwimu hizo zilizotolewa Jumatatu unaonyesha kuwa pato la ongezeko la thamani la viwanda na makampuni makubwa ya viwanda lilipaa kwa asilimia 4.8 mwaka hadi mwaka katika robo ya tatu, ikiwa ni asilimia 4.1 kwa kasi zaidi kuliko robo ya pili.

Huku shughuli za kiuchumi kwa ujumla zikiimarika, soko la wanunuzi bidhaa limeongezeka katika robo ya tatu. Jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa za walaji nchini China iliongezeka kwa asilimia 3.5 kuliko ile ya robo ya tatu ya mwaka jana, na hivyo kurudisha nyuma upungufu wa asilimia 4.6 uliojitokeza katika robo ya pili.

Uwekezaji wa mali zisizohamishika uliendeleza kasi ya ukuaji katika robo ya tatu, ukipanda kwa asilimia 5.7 kutoka kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, na kupanda kwa asilimia 1.5 kutoka robo ya pili.

Katika kipindi cha Januari-Septemba, uwekezaji katika sekta ya viwanda ulipanda kwa asilimia 10.1 kuliko mwaka jana huku uwekezaji katika viwanda na huduma za teknolojia ya juu ukiendelea kupanuka kwa kasi, na kupanda kwa asilimia 23.4 na asilimia 13.4, mtawalia.

"Kwa ujumla, uchumi wa China umeweza kuondokana na athari mbaya zinazosababishwa na mambo yasiyotarajiwa, na viashiria vikuu vikibaki ndani ya viwango vya kuridhisha na sababu nzuri zikikusanyika," NBS imesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>