Lugha Nyingine
Viongozi wa vyama na serikali za nchi mbalimbali wampongeza Xi Jinping kwa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC
Viongozi wa vyama na serikali za nchi mbalimbali wametoa salamu za pongezi kwa Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC.
Akitoa pongezi hizo Rais Vladimir Putin wa Russia alisema kufanyika kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kumeonyesha heshima ya kisiasa ya Xi Jinping na mshikamano mkubwa wa CPC chini ya uongozi wake. Maamuzi mbalimbali yaliyotolewa kwenye Mkutano huo yataisaidia China kutimiza lengo lake kubwa la maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuzidi kuinua hadhi ya China duniani. Amesema anapenda kuendelea kufanya mazungumzo ya kiujenzi na ushirikiano wa karibu na Xi Jinping, na kuendeleza zaidi uhusiano wa wenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi mbili.
Mwenyekiti wa chama cha ANC ambaye pia ni Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alimpongeza Xi Jinping na kuutakia kila la heri uongozi wa Kamati Kuu ya awamu mpya ya CPC. Amesema Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC umetoa mwelekeo kwa CPC na China katika kufunga safari mpya. Chama cha ANC kinathamini sana uhusiano wake na CPC, na chini ya uongozi wa Xi Jinping, uhusiano kati ya vyama hivi viwili umezidishwa siku hadi siku. Ramaphosa ameeleza imani yake kuwa CPC itashirikiana na wadau wanaohimiza maendeleo ya dunia na kuendelea kuhimiza utimizaji wa usawa, haki na maendeleo ya amani duniani.
Mwenyekiti wa Chama cha Justicialist cha Argentina na rais Alberto Fernández amesema kuwa chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Xi Jinping, China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na mapambano dhidi ya COVID-19, ambayo yameboresha sana maisha ya Wachina na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine mbalimbali. Anamtakia Katibu Mkuu Xi Jinping aiongoze China isonge mbele kwenye safari ya kutafuta maendeleo na ustawi, na kupata mafanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Harakati za Ukombozi wa Watu wa Sudan SPLM cha Sudan Kusini, ambaye pia ni Rais wa nchi hiyo Salva Kiir amekishukuru chama cha CPC kwa uungaji mkono wake wa muda mrefu kwa chama cha SPLM na nchi ya Sudan Kusini. Ameahidi kwamba yeye na Chama chake watashirikiana kwa karibu na katibu mkuu Xi Jinping na CPC ili kuhimiza maendeleo endelevu ya uhusiano wa kirafiki kati ya vyama hivyo viwili, ili kunufaisha vyama viwili, nchi mbili na watu wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma