Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping apokea nishani ya ngazi ya juu zaidi ya Urafiki iliyotolewa na rais Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan
Tarehe 15, Septemba kwa saa za Samarkand, rais Xi Jinping wa China akipokea nishani hiyo iliyotolewa na rais Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa cha Samarkand, Uzbekistan. (Xinhua/Ding Haitao)
Tarehe 15, Septemba kwa saa za Samarkand, rais Xi Jinping wa China alipokea nishani ya ngazi ya juu zaidi ya Urafiki iliyotolewa na rais Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa cha Samarkand, Uzbekistan.
Nishani ya ngazi ya juu zaidi ya Urafiki ni heshima ya juu zaidi inayotolewa na Uzbekistan kwa watu wa nchi za nje, ikilenga kusifu watu waliotoa mchango maalum kwa ajili ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya Uzbekistan na nchi nyingine, kutatua matatizo makubwa ya kimataifa na kikanda, na kuchangia maendeleo ya nchi ya Uzbekistan. Hii ni mara ya kwanza kwa nishani hiyo kutolewa tangu ilipowekwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma