久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Rais Xi Jinping wa China apokea nishani ya Tai wa Dhahabu iliyotolewa na Rais wa Kazakhstan, Tokayev

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2022

Rais Xi Jinping wa China akipokea Nishani ya Tai wa Dhahabu iliyotolewa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev kwenye Ikulu ya Rais ya Ak Orda mjini Nur-Sultan, Kazakhstan, Septemba 14, 2022. Tuzo ya Nishani ya Tai wa Dhahabu ni ya juu zaidi nchini Kazakhstan na hutolewa na rais wa nchi hiyo. (Xinhua/Rao Aimin)

NUR-SULTAN--Rais wa China Xi Jinping Jumatano alasiri alipokea nishani ya Tai wa Dhahabu iliyotolewa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika Ikulu ya Rais ya Ak Orda huko Nur-Sultani.

Katika kasri la kifahari lililopambwa kwa marumaru, bendera za taifa za China na Kazakhstan zilipangwa vizuri, na kukijaza chumba hali ya ukarimu na ya heshima.

Kabla ya kutolewa kwa nishani hiyo, Tokayev alitoa hotuba. Katika hotuba yake, ameweka bayana kuwa ziara ya Rais Xi Jinping wa China, ni heshima kubwa kwa Kazakhstan.

Rais Xi ni kiongozi mkuu wa kweli ambaye anaungwa mkono kwa moyo wote na watu wa China, Tokayev amesema, huku akiongeza kuwa chini ya uongozi wa Xi, China imepata maendeleo makubwa, kuondoa umaskini uliokithiri, na kujenga jamii yenye ustawi katika mambo yote na taifa la China linaandamana katika safari mpya kuelekea kwenye ustawi mkubwa.

Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wenye busara wa Xi, China itatimiza lengo kuu la kujenga kikamilifu nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa kama ilivyopangwa.

“Xi amependekeza mipango mikubwa ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na ujenzi wa jumuiya ya bindamu yenye mustakabali wa pamoja, na ametoa mchango mkubwa katika kujenga aina mpya ya uhusiano wa kimataifa,” Tokayev amesema, na kuongeza kuwa, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia ambayo kwa pamoja yametolewa na Rais Xi yana umuhimu maalum wa kimkakati katika kutatua hatari na changamoto zinazokabili dunia ya leo.

Tokayev pia amepongeza sana jukumu la kihistoria na mchango wa ajabu wa Xi katika kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili na katika kukuza uhusiano kati ya Kazakhstan na China, na ameweka bayana kuwa ziara ya Xi itakuwa na umuhimu katika historia ya uhusiano kati ya Kazakhstan na China.

“Kazakhstan iko tayari kushirikiana na China ili kuendeleza ustawi na maendeleo ya pamoja ya nchi hizo mbili, kutoa mchango kwa ajili ya ustawi wa watu wa pande mbili, na kuungana mkono ili kujenga mustakabali mzuri zaidi,” amesema.

Tokayev ametoa nishani ya Tai wa Dhahabu kwa Xi. Wakuu hao wa nchi walipiga picha ya pamoja.

Akitoa hotuba yake baada ya kupokea nishani hiyo, Xi ameelezea kupewa kwake nishani hiyo kama udhihirisho wa umuhimu mkubwa wa sehemu ya Kazakhstan katika uhusiano kati ya China na Kazakhstan na akiba ya nia njema ya watu wa Kazakhstan kwa watu wa China.

Katika miongo mitatu iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya China na Kazakhstan umeendelea kukua kwenye kiwango cha juu, Xi amesema, na kuongeza kuwa pande hizo mbili zimeimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, ushirikiano umeimarika katika sekta mbalimbali, juhudi za kuhimiza ubora wa hali ya juu wa ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” zimeleta matokeo yenye matunda, na pande hizo mbili pia zimeshiriki katika uratibu wa karibu katika masuala ya kimataifa, ambayo yote yametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi wa nchi zote mbili na kuweka msukumo mkubwa katika amani na utulivu wa kikanda.

“Mustakabali mwema unakuja kwa urafiki wa kudumu, ushirikiano wenye manufaa na ustawi wa pamoja kati ya nchi hizo mbili,” Xi amesema.

Xi amesema anathamini sana nishani hiyo , ambayo inaonesha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili, na ameelezea imani yake kwamba kwa juhudi za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Kazakhstan utapanda juu na kuruka mbali kama tai wa dhahabu na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Nishani ya Tai wa Dhahabu ni tuzo ya juu zaidi ya Kazakhstan iliyotolewa kwa watu waliotoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa ya Kazakhstan na uhusiano wa nje wa kirafiki.

Rais Xi Jinping wa China akipokea Nishani ya Tai wa Dhahabu iliyotolewa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika Ikulu ya Rais ya Ak Orda mjini Nur-Sultan, Kazakhstan, Septemba 14, 2022. (Xinhua/Rao Lengo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>