Lugha Nyingine
Mipango inayopendekezwa na China yajikita katika maendeleo na usalama wa Dunia
BEIJING - Kuanzia leo Jumatano hadi Ijumaa, Rais Xi Jinping wa China atahudhuria kwenye mkutano wa 22 wa Baraza la Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Samarkand, Uzbekistan, na kufanya ziara za kiserikali katika nchi za Kazakhstan na Uzbekistan.
Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai unafanyika wakati ambapo Dunia inashuhudia athari za pamoja za janga la UVIKO-19 ambalo halijapata kuonekana katika karne moja iliyopita, mwelekeo wa kukwama kwa utandawazi na mambo mengine yenye changamato, na mfumo wa usimamizi wa uchumi wa Dunia unakabiliwa na changamoto.
Rais wa China Xi Jinping amependekeza mipango na mapendekezo kadhaa muhimu kwa ajili ya maendeleo na usalama wa Dunia, akichangia hekima na bidhaa ya umma ya China katika kutatua matatizo yanayowakabili binadamu sasa, jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe na jumuiya ya kimataifa, zikiwemo nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai.
Maendeleo na Usalama kwa wote
Maendeleo na usalama ni masuala yanayofuatiliwa kwa karibu na nchi zote na vipaumbele vya juu vya usimamizi wa Dunia.
Katika taarifa iliyotolewa kwa njia ya video kwenye mjadala mkuu wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba, 2021, Rais Xi alipendekeza Mpango wa Maendeleo ya Dunia (GDI) ili kuelekeza maendeleo ya kimataifa kuelekea hatua mpya ya ukuaji wenye uwiano, uratibu na shirikishi wakati ambapo Dunia inakabiliana na athari kubwa za UVIKO-19.
Sudheendra Kulkarni, mwenyekiti wa zamani wa Taasisi ya Utafiti ya Waangalizi wa India, anasema maendeleo na usalama ni "pande mbili za sarafu moja na zote hazigawanyiki."
"Hakuna nchi inayoweza kupata usalama ikiwa nchi nyingine hazina usalama, na hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo ikiwa maendeleo ya nchi nyingine yako hatarini. Ni lazima tuzingatie usalama na maendeleo katika mazingira ya kimataifa," Kulkarni anasema.
Kuhimiza maendeleo ya pamoja
Dunia kwa sasa inapitia mabadiliko makubwa na janga la UVIKO-19, yote mawili hayajawahi kuonekana katika karne moja iliyopita, wakati uchumi wa Dunia bado unapambana dhidi ya upepo mkubwa kwenye njia yake ya kufufuka.
Licha ya vikwazo hivyo vikubwa kwa maendeleo ya Dunia, China daima ni mjenzi wa amani ya Dunia, mchangiaji wa maendeleo ya kimataifa, mtetezi wa utaratibu wa kimataifa na mtoa huduma wa bidhaa za umma.
Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, lililopendekezwa na Rais Xi miaka tisa iliyopita, limekuwa mpango maarufu zaidi wa umma duniani. Zaidi ya hayo, China imekuwa ikijitahidi sana kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa watu wengi zaidi iwezekanavyo duniani kote.
Kuhusu ushirikiano mkubwa wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai pamoja na ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Xi alisema alipohutubia mkutano wa 21 wa Baraza la Wakuu wa Nchi za SCO Mwezi Septemba, 2021, "Ushirikiano wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' unatoa jukwaa muhimu la kuhimiza maendeleo ya pamoja kwa ajili yetu wote."
Mustakabali wa pamoja wa binadamu
Kwa muda mrefu Rais Xi amekuwa akitoa wito wa kujenga jumuiya ya bindamu yenye mustakabali wa pamoja. Akihutubia mkutano wa 21 wa Baraza la Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mwaka jana kwa njia ya video, Xi alitoa mapendekezo matano kuhusu kujenga "jumuiya iliyo karibu zaidi na yenye mustakabali wa pamoja."
Alisema, nchi za jumuiya hiyo zinahitaji kufuata safari ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kudumisha usalama wa pamoja, kuhimza uwazi na utangamano, kuongeza mwingiliano na kufundishana na kudumisha usawa na haki.
Kwa miaka mingi, Xi ametimiza maono yake kuhusu ushirikiano wa jumuiya hiyo, na kuhamasisha jumuiya hiyo kukua na kuwa mfano wa kuigwa katika ujenzi wa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma