Lugha Nyingine
Xi ampongeza Mfalme Charles III kwa kutangazwa rasmi kuwa mfalme wa Uingereza
(CRI Online) Septemba 13, 2022
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Mfalme Charles III kwa kutangazwa rasmi kuwa mfalme wa Uingereza.
Akielezea kuwa mwaka huu nchi hizo mbili zinaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya mabalozi, rais Xi amesema yuko tayari kushirikiana na Mfalme Charles III ili kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, kupanua mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana, na kuendelea zaidi kubadilishana maoni katika masuala ya kimataifa, ili kuleta manufaa kwa nchi hizo mbili na watu wao pamoja na kuchangia amani na maendeleo ya dunia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma