Lugha Nyingine
Rais Xi wa China atuma salamu za pongezi kwa Rais mteule wa Kenya Ruto
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2022
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii alituma salamu za pongezi kwa William Samoei Ruto kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya.
Katika salamu zake, Xi ameeleza kuwa China na Kenya zinafurahia urafiki wa muda mrefu, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali umekuwa na matokeo mazuri katika miaka ya hivi karibuni.
Akiweka bayana kwamba anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kenya, Xi amesema yuko tayari kufanya juhudi za pamoja na Ruto kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati na wa kina kati ya China na Kenya, ili kunufaisha nchi hizi mbili na wananchi wao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma