久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mtazamo wa Uchumi wa EU wafifishwa na mfumuko wa bei, mgogoro wa nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 17, 2022

BRUSSELS - Mfumuko wa bei kote Ulaya umefikia rekodi nyingine ya juu zaidi kihistoria na mgogoro wa nishati uliodumu kwa miezi kadhaa hauonyeshi dalili ya kupungua, bali kudhoofisha manunuzi ya bidhaa na kutia giza matarajio ya kiuchumi.

Umoja wa Ulaya (EU) umezitaka nchi wanachama wake kupunguza mahitaji ya nishati, hatua ambayo ufanisi wake unatiliwa shaka. Mtazamo wa kiuchumi wa umoja huo, unaokumbwa na ongezeko la mfumuko wa bei na mgogoro wa nishati, umezidi kuwa mbaya huku kukiwa na hatari zinazoendelea za kushuka kwa uchumi.

Madhara ya kupanda kwa bei ya nishati yanaonekana kila mahali barani Ulaya, kutokana na sababu kadhaa hasi, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa ufanisi wa vikwazo vikubwa dhidi ya Russia na kuongezeka kwa viwango vya riba nchini Marekani.

Mfumko wa bei juu, manunuzi ya bidhaa chini

Mteja akipita kwenye rafu tupu za mafuta ya kupikia kwenye moja ya supamaketi mjini Paris, Ufaransa, Machi 26, 2022. (Xinhua/Gao Jing)

Wakazi wa Ulaya sasa wanapaswa kukabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha na kupungua kwa uwezo halisi wa kununua, jambo ambalo limepunguza imani yao katika manunuzi.

Wakati huo huo, kuongezeka kwa gharama za nishati pia kumesababisha kushuka kwa pato la viwanda na kufungwa kwa shughuli za kampuni nyingine zinazotumia nishati nyingi, na kusababisha athari mbaya zaidi kwa uchumi wa Ulaya.

Kwa mujibu wa makadirio mapya kutoka Shirika la Takwimu la Ulaya, Eurostat, Mwezi Juni, mauzo katika eneo linalotumia sarafu ya euro yalishuka kwa asilimia 1.2 mwezi hadi mwezi, au kwa asilimia 3.7 mwaka hadi mwaka.

Kiasi cha biashara ya rejareja mwezi Juni katika Umoja wa Ulaya kilipungua kwa asilimia 1.3 ikilinganishwa na Mwezi Mei, au kwa asilimia 2.8 ikilinganishwa na Mwezi Juni 2021.

Gharama ziliongezeka wakati ambapo mauzo ya rejareja yalipungua.

Mashaka bado yanabaki kwenye uchumi wa EU

Ili kuhakikisha usambazaji wa nishati katika msimu wa baridi unaokaribia, EU inahimiza nchi wanachama wake kuokoa matumizi ya nishati na kuboresha ufanisi wa nishati. Makubaliano yaliyofikiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kupunguza mahitaji ya gesi msimu huu wa baridi kwa asilimia 15 yalianza kutekelezwa mwezi huu. Hata hivyo, maswali yanabaki ikiwa makubaliano hayo yatafanya kazi.

Picha iliyopigwa Agosti 1, 2022 ikionyesha mandhari ya usiku ya ukumbi wa jiji huko Hanover, Ujerumani. Baadhi ya miundombinu maarufu kote nchini Ujerumani imepunguza mwangaza wake wa usiku ili kuokoa umeme. (Picha na Joachim Sielski/Xinhua)

Kwa upande mmoja, kutokana na uwezo usio sawa wa kuhifadhi na usambazaji wa gesi kati ya nchi wanachama wa EU, tofauti juu ya makubaliano hayo bado zinadumu ndani ya EU.

Nchi ya Hungary, kwa mfano, ilitilia shaka uhalali wa sheria za Umoja wa Ulaya zinazoathiri mchanganyiko wa nishati au usalama wa nishati wa nchi. Poland ilielezea msingi wa kisheria wa mpango huo kuwa ni "kasoro," ikisema kuwa maamuzi yanayoathiri mchanganyiko wa nishati ya nchi wanachama wa EU yanapaswa kuchukuliwa kwa idhini ya pamoja kutoka kwa nchi zote.

Kwa upande mwingine, wachambuzi wa mambo wanatilia shaka kama kufikiwa kwa lengo la kupunguza asilimia 15 ya gesi asilia kutahakikisha Ulaya kupita msimu huo wa baridi.

Picha iliyopigwa Tarehe 28 Juni 2022 ikionyesha eneo la mradi wa uendelezaji gesi asilia wa Midia katika Kijiji cha Vadu kwenye pwani ya Bahari Nyeusi, Kusini Mashariki mwa Romania. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

Nathan Piper, mchambuzi wa masuala ya nishati za mafuta na gesi wa Investec, ambalo ni shirika la benki la kimataifa, anasema kuna "gharama kubwa ya kisiasa na kiuchumi" kwani EU inaangalia kupunguza utegemezi wake kwa gesi ya Russia, na gharama hiyo inadhihirishwa kupitia misamaha ya nchi wanachama wake, jambo ambalo linaweza kupunguza athari za hatua hizo.

Mtazamo wa kiuchumi wenye giza

Ingawa uchumi wa Ulaya ulikua katika robo ya pili, wachambuzi wanasema kwamba hii inaweza kuwa hali ya mwisho ya mdororo wa uchumi unaotarajiwa katika nusu ya pili ya mwaka huu huku athari za kufufua uchumi zikidhoofika hatua kwa hatua.

Picha iliyopigwa Juni 1, 2022 ikionyesha sanamu ya nembo ya Euro huko Frankfurt, Ujerumani. (Xinhua/Lu Yang)

Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) limesema katika ripoti yake mpya ya Viashiria Vikuu vya Mchanganyiko (CLIs) kwamba vikiwa "vimeshushwa na mfumuko wa bei wa juu wa kihistoria, imani ya chini ya wanunuzi wa bidhaa na kushuka kwa fahirisi za bei ya hisa, CLI bado hazijabadilika na zinaendelea kutarajia kupoteza kasi ya ukuaji katika uchumi mkubwa zaidi wa OECD."

CLIs, ambavyo vimeundwa kukadiria mabadiliko kwenye shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi sita hadi tisa ijayo, vinaendelea "kuashiria kuzorota kwa mtazamo wa kiuchumi katika nchi nyingi zenye uchumi mkubwa," imesema ripoti hiyo.

"Hali hii ipo kwa nchi za Canada, Uingereza na Marekani, na pia katika eneo linalotumia sarafu ya euro kwa ujumla ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani na Italia," imesema ripoti. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>