Lugha Nyingine
Kasi ya kufufuka kwa uchumi wa China yaendelea Mwezi Julai
Msemaji wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS), Fu Linghui (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China kuhusu viashirio vingi muhimu vya kiuchumi vya China kwa Mwezi Julai, hapa Beijing, China, Agosti 15, 2022. (Xinhua/Chen Yehua)
BEIJING - Uchumi wa China umeendelea kudumisha mwelekeo wake wa kuimarika Mwezi Julai huku viashiria vikuu vya uchumi vikirekodi ukuaji thabiti licha ya milipuko ya virusi vya corona na halijoto kali.
Takwimu kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) Jumatatu wiki hii zilionyesha kuwa Pato la thamani ya uzalishaji la viwanda nchini China lilipanda kwa asilimia 3.8 Mwezi Julai na kuongezeka kwa asilimia 0.38 kuliko kipindi cha Mwezi Juni.
Mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yalipanda kwa asilimia 2.7 mwezi uliopita, huku mauzo ya bidhaa zinazoboresha kama vile vito na vyombo vya umeme nyumbani yakipanuka kwa haraka.
Takwimu hizo za NBS zimeonyesha kuwa, viashiria vingine vikuu vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na fahirisi ya uzalishaji wa huduma na uwekezaji wa mali zisizohamishika pia vilionyesha ukuaji.
Kutokana na kuimarika kwa uchumi, kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichofanyiwa utafiti kiliendelea kushuka Mwezi Julai, kutoka asilimia 5.5 Mwezi Juni hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi uliopita.
“Kuendelea kuimarika kwa uchumi mnamo Julai hakukuja kwa urahisi kwani China ililazimika kukabiliana na milipuko ya mara kwa mara ya virusi vya corona na hali joto ya juu ya hewa katika mikoa mingi,” Msemaji wa NBS Fu Linghui amewaambia waandishi wa habari kwenye mkutano na waandishi wa habari uliondaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China.
Fu amesema kuwa uboreshaji na mageuzi katika uchumi wa China pia ulisonga mbele.
Mnamo Mwezi Julai, mapato yanayotokana na mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya na seli za nishati za jua yaliongezeka kwa asilimia 112.7 na asilimia 33.9.
Katika kipindi cha Januari hadi Julai, thamani iliyoongezwa ya utengenezaji kwa teknolojia ya juu iliongezeka kwa asilimia 9, na uwekezaji katika viwanda vya teknolojia ya juu ulipanda kwa asilimia 20.2.
"Hata hivyo, uchumi bado uko katika mchakato wa kufufuka, na mahitaji ya soko yanatakiwa kupanuka," Fu amesema, huku akiongeza kuwa msingi wa kufufua uchumi unahitaji kuwekewa mkazo.
Takwimu kutoka Benki Kuu ya China zinaonesha kuwa, ufadhili mpya wa kijamii ulioongezwa, ambacho ni kipimo cha fedha ambazo watu binafsi na mashirika yasiyo ya kifedha hupokea kutoka kwenye mfumo wa mambo ya fedha, ulikuwa yuan bilioni 756.1 (kama dola za Kimarekani bilioni 112.16) mwezi uliopita, ikiwa ni kiwango cha chini cha yuan bilioni 319.1 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.
Fu ameeleza matarajio yake kuwa manunuzi ya bidhaa kwa kaya yatarejea hatua kwa hatua kutokana na sera zaidi za kuzuia na kudhibiti janga la corona na kuunga mkono matumizi. Hasa, sera za upendeleo kwa manunuzi ya magari na vifaa vya nyumbani zitachochea ukuaji wa mauzo ya bidhaa.
Kadiri vizuizi vya minyororo ya viwanda na ugavi vinapoendelea kushughulikiwa hatua kwa hatua, viwanda muhimu kama vile vya uundaji wa magari vinaanza tena uzalishaji wa kawaida, ambao utaendelea kuwa na jukumu la kusaidia ukuaji wa viwanda vya China.
"Kwa juhudi za pamoja, kasi ya kufufuka kwa uchumi inatarajiwa kuendelea," Fu amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma