Lugha Nyingine
Kenya yaanza kusafirisha maparachichi freshi kwenye soko la China
Shehena ya maparachichi freshi yanayolimwa nchini Kenya na kutarajiwa kufikishwa kwenye soko la China imeanza kusafirishwa jana Jumanne.
Kwenye hafla iliyofanyika kabla ya kusafirishwa shehena hiyo ambayo imehudhuriwa na maafisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia na watendaji wa sekta hiyo, David Osiany, Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na maendeleo ya makapuni amesema kwa kusafirisha maparachichi freshi nchini China, mapato ya fedha za kigeni ya Kenya yanatarajiwa kuongezeka na kuibua uhai wa uchumi nchini humo.
Idara ya Kuu ya forodha ya China ikishirikiana na Huduma ya Ukaguzi wa Afya ya Mimea ya Kenya wamekuwa wakihusika katika kuthibitisha usalama na vigezo vya ubora vya maparachichi yanayolimwa na wenyeji wa Kenya kabla ya kusafirishwa na kuletwa nchini China.
Kenya imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kusafirisha maparachichi freshi nchini China katika hatua ya kuongeza kasi zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma