Lugha Nyingine
IMF yaidhinisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 235.6 kuunga mkono bajeti ya Kenya
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2022
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limepitisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 235.6 kwa Kenya.
Shirika hilo limesema katika taarifa yake kuwa, fedha hizo zimetolewa ili kuunga mkono Kenya kukabiliana na tishio la madeni, kujibu athari za janga la COVID-19 na changamoto za dunia zinazotokana na mgogoro unaoendelea nchini Ukraine, na pia kuunga mkono serikali na mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini humo.
Taarifa hiyo imesema, uchumi wa Kenya umefufuka kwa nguvu katika mazingira magumu na unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.7 mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma